Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, akisalimiana na Kiongozi wa Machifu wa Botswana Chifu Gaborone wa kabila la Batlokwa walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024.
Kiongozi wa Machifu wa Botswana Chifu Gaborone wa kabila la Batlokwa akizungumza na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (hawako pichani) walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024. Kiongozi wa wa Chama cha Real Alternative Bw. Gaontebale Mokgosi akizungumza kikao cha machifu na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (hawako pichani) walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024.
Baadhi ya Machifu wa Botswana katika picha ya pamoja na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (hawako pichani) walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024.***************
Mkuu wa
Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika
(SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, amekutana na kuzungumza na machifu kutoka koo
mbalimbali za nchini Botswana katika kikao kilichofanyika jijini Gaborone
tarehe 27 Oktoba 2024 ikiwa ni sehemu ya vikao ambavyo SEOM imekuwa ikifanya na
wadau mbalimbali wa uchaguzi nchini humo.
Mhe. Pinda ametumia
kikao hicho kuwajulisha machifu hao kuhusiana na kazi ya uangalizi wa uchaguzi
mkuu wa Botswana kuanzia maandalizi, mwenendo wake na jinsi mambo yalivyo wakati
huu wa uchaguzi ikiwa ni kutekeleza jukumu la Uangalizi kwa kuzingatia misingi
na miongozo ya uchaguzi wa kidemokrasia iliyowekwa na SADC.
Aliwaambia
machifu hao kuwa SEOM imekuwa ikikutana na wadau mbalimbali na kuzungumza nao moja kwa moja na hivyo kupata
picha halisi ya jinsi mwenendo na maandalizi ya uchaguzi huo yalivyo na
kuongeza kuwa SEOM imepeleka waangalizi wake katika majimbo yote ya uchaguzi
ili kuangalia hali inavyokwenda, itakavyokuwa siku ya uchaguzi na baada ya
uchaguzi.
Akizungumza katika
kikao hicho Kiongozi wa Machifu wa Botswana Chief Gaborone toka kabila la
Batlokwa alisema wao kama machifu wana jukumu la kuhakikisha koo zao hazigawanyiki
licha ya kuwa wananchi wao ni wafuasi wa vyama vya siasa na kwa kufanya hivyo amani na usalama vitaendelea kuwepo katika maeneo
yao.
Alisema wao
wakiwa viongozi wa kimila na kijadi nchini humo wana wajibu wa kuwahimiza
wananchi kushiriki katika michakato ya siasa ili waweze kuchagua viongozi wa
kisiasa ambao wataongoza nchi kwa kipindi husika.
Amesema wao
sio wanasiasa ila wanashirikiana na viongozi serikali kuhakikisha wananchi wanashiriki
kikamilifu katika shughuli za siasa kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na
miongozo iliyopo akitolea mfano wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Botswana ilivyowafuata
na kuwajulisha juu ya juu ya kufanyika kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura na
kuwaomba kuwasaidia kufikisha ujumbe huo wa uandikishaji wapiga kura kwa
wananchi kwenye maeneo yao.
Naye Chifu Lotlamoreng
kutoka kabila la Barolong amesema kama chifu akitaka kujihusisha moja kwa moja
na masuala ya siasa ni lazima aondoke katika kazi ya uchifu ili aweze kuwa huru
kujihussiha na masuala ya siasa nchini humo.
Wamesema machifu
hawajazuiwa kugombea nafasi za siasa ila wanatakiwa wajue kuwa ukiamua kugombea
na kushiriki kama mgombea unatakiwa kuondoka katika ofisi ya chifu ili kuepuka
mgogoro wa maslahi na sheria Sheria ya Machifu ya mwaka 2008 ambayo inawatambua
machifu na Ofisi zao nchini Botswana.
Ameongeza
kuwa katiba ya Botswana pia inatambua Ofisi ya Machifu na inawatambua machifu
hao ambo wako zaidi ya 500 wakiwamo machifu wananwake ambao wanakaribia 100.
Katika
mkutano mwingine, SEOM ilikutana na Kiongozi wa wa Chama cha Real Alternative
Bw. Gaontebale Mokgosi ambaye alionyesha
wasiwasi kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo ambayo yamefanywa na Tume Huru ya
Uchaguzi (IEC), akitaja kuchelewa kwa uchapishaji wa karatasi za kupigia kura
kama mfano wa mandalizi duni ya uchaguzi huo na wanadhani kuwa IEC haiko tayari
kuendesha uchaguzi huru na wa na haki.
Chama hicho
kilisisitiza umuhimu wa kuongeza utoaji wa elimu ya wapiga kura na kupendekeza
kuwa IEC inapaswa kushirikiana kwa karibu na vyama vya siasa nchini Botswana
ili kuhamasisha watu wengi zaidi kushiriki zoezi la kuandikisha wapiga kura na
kujitokeza kupiga kura. Pia walisisitiza umuhimu wa ofisi ya ushirikiano wa
vyama vya kisiasa kutakiwa kufanya kazi zaidi mwaka huu wa uchaguzi kinyume na
ilivyokuwa kwakuwa ofisi hiyo ina jukumu muhimu la kuunganisha IEC, vyama vya
kisiasa, na raia kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment