Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia
wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 53 wa Mwaka wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola
Kanda ya Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini
Arusha. Tarehe 03 Oktoba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 53 wa Mwaka wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha. Tarehe 03 Oktoba 2024.Sehemu ya washiriki wa Mkutano
wa 53 wa Mwaka wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika unaofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha. Tarehe 03 Oktoba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na
viongozi mbalimbali wakielekea katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini
Arusha wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 53 wa Mwaka wa Mabunge ya Jumuiya ya
Madola Kanda ya Afrika. Tarehe 03 Oktoba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na viongozi mbalimbali katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 53 wa Mwaka wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika. Tarehe 03 Oktoba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Maspika mbalimbali wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika mara baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa 53 wa Mwaka wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha. Tarehe 03 Oktoba 2024
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema katika kushughulikia changamoto za Kimataifa za Uhaba wa Chakula, Mabadiliko ya tabianchi pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana inahitajika juhudi za pamoja za wadau wote na uwepo wa amani endelevu Barani Afrika.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na viongozi mbalimbali katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 53 wa Mwaka wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika. Tarehe 03 Oktoba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Maspika mbalimbali wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika mara baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa 53 wa Mwaka wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha. Tarehe 03 Oktoba 2024
***************
Amesema Mabunge Barani Afrika yana nafasi ya kipekee
katika kufikia malengo hayo kwa kutunga sheria madhubuti na kufanya uangalizi.
Makamu
wa Rais ametoa wito kwa mkutano huo kutumika katika kubadilishana mbinu bora na
uzoefu wa mataifa kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa ufanisi zaidi
sambamba na azimio la kumaliza migogoro na vita Barani Afrika.
Kuhusu
ajira kwa vijana, Makamu wa Rais amesema Mabunge yana wajibu wa kueleza
changamoto za vijana, kuweka mbele hatua za kuchukuliwa na kushauri serikali
katika kubuni programu za ajira kwa vijana na kuhakikisha kwamba zinafadhiliwa
ipasavyo kupitia bajeti ya taifa na ushirikiano wa wadau mbalimbali.
Ameongeza
kwamba Mabunge yanapotunga sheria na kufanya usimamizi yanahitaji kufanya kazi
na serikali ili kukuza sera na programu zinazounga mkono ajira na ufadhili wa
kibunifu kwa programu za ujasiriamali kwa vijana.
Kuhusu
Mabadiliko ya tabianchi, Makamu wa Rais amesema Wabunge wana wajibu wa
kuhakikisha hatua Madhubuti zinachukuliwa na serikali pamoja na wadau wengine
ili kukabiliana na janga hilo kupitia utekelezaji wa hatua Madhubuti ikiwemo za
matumizi ya teknolojia za kijani.
Pia amesema licha ya kutenga bajeti ya
uhifadhi mazingira kitaifa ni muhimu mabunge kuharakisha uidhinishaji na
utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ikiwemo Mkataba wa Paris pamoja na
Marekebisho ya Doha kwa Itifaki ya Kyoto.
Aidha
Makamu wa Rais amesema Mabunge pia yanapaswa kusimamia utekelezaji wa mipango
iliyoamuliwa kitaifa ili kupunguza uzalishaji wa gesi joto pamoja na kuimarisha
uwazi na uwajibikaji wa hatua na utoaji wa taarifa kuhusu mabadiliko ya
tabianchi.
Halikadhalika kuwa mstari wa mbele katika ajenda ya mabadiliko ya
tabianchi kwa kuandaa mijadala yenye ubora ili kukuza uelewa na hatua za
kuchukua haraka kuzuia uharibifu wa mazingira kitaifa na kimataifa.
Vilevile
akizungumzia uhaba wa chakula, Makamu wa Rais amesema licha ya uwezo mkubwa wa
kilimo barani Afrika, bado wananchi wanakabiliwa na ukosefu wa chakula.
Ametoa
rai kwa Mabunge barani Afrika kuweka mkazo katika kuimarishwa kwa uwekezaji wa
umma katika sekta ya kilimo na sekta shiriki kwa kutenga bajeti kwa ajili ya
kuongeza usambazaji na upatikanaji wa pembejeo za kilimo na huduma za
miundombinu.
Pia
Makamu wa Rais amesema Mabunge yana jukumu la kutunga sheria zitakazosaidia
usalama wa chakula na kuwezesha uwekezaji katika sekta ya kilimo na sekta
shirikishi.
Amesisitiza umuhimu wa miundombinu ya umwagiliaji, upatikanaji wa
mikopo ya kilimo, mbegu bora, huduma za ugani, maghala ya uhifadhi mazao, huduma
za miundombinu vijijini pamoja na upatikanaji wa masoko.
0 comments:
Post a Comment