Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio leo tarehe 06 Oktoba, 2024 ameongoza kikao cha maandalizi cha Wataalam kutoka Tanzania watakaoshiriki Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika (Afrika Oil Week). Kikao kimefanyika Jijini Cape Town nchini Afrika Kusini.
Kongamano hilo litafanyika kuanzia tarehe 07 hadi 10, Oktoba, 2024 nchini humo.
Maudhui ya Kongamano hilo ni pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya Mafuta, Gesi Asilia na Nishati Mbadala katika Bara la Afrika.
0 comments:
Post a Comment