TIMU za michezo ya mpira wa miguu, netiboli na kuvutana kwa kamba zimetoana jasho kwa kuonesha burudani safi kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa mikoa iliyofanyika leo Septemba 20, 2024 kwenye viwanja na Jamhuri, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) vilivyopo katika Kampasi ya Edward Moringe ( Kampasi Kuu) na Kampasi ya Solomon Mahlangu ( Mazimbu), Shule ya Sekondari ya Morogoro na Chuo cha Teknolojia ya Ujenzi ambapo zamani kikijulikana Chuo cha Ujenzi.
Katika mchezo wa mpira wa netiboli uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri A na B timu ya Tume za Haki za Binadamu na Utawala Bora iliwafunga Bodi ya Pamba kwa magoli 29-2 huku Ofisi ya Bunge iliwachapa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa magoli 31-19 wakati Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wamewashinda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa magoli 35-18.
Katika mechi nyingine timu ya Hazina wamewaliza RAS Dar es Salaam kwa magoli 41-6 nao Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamewachapa Wizara ya Ujenzi magoli 30-16; huku Wizara ya Maliasili na Utalii wamewafunga Wizara ya Uchukuzi kwa magoli 41-15 na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu waliwashinda Wizara ya Nishati kwa magoli 41-26; nao Ofisi ya Rais Ikulu wamewaadhibu Wizara ya Mambo ya Ndani kwa magoli 51-2; na Mahakama waliwachapa Maadili kwa mabao 42-19.
Kwa upande wa mpira wa miguu timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliwafunga Wizara ya Viwanda na Biashara kwa magoli 3-1; huku RAS Manyara walitoshana nguvu na BRELA kwa sare ya bao 1-1; nao Mahakama waliwachapa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa magoli 5-0 na OSHA waliwafunga Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi kwa magoli 2-1.
Katika mechi nyingine Wizara ya Ardhi waliwaliza RAS Kigoma kwa magoli 2-1; nao RAS Mara waliwashinda jamaa zao RAS Lindi kwa magoli 3-0; huku Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora waliwafunga Wizara ya Ujenzi kwa bao 1-0; nao TARURA waliwaliza RAS Tanga kwa magoli 4-1; huku Hazina mabingwa watetezi waliwachapa bila huruma Tume ya Maadili ya Umma kwa magoli 10-0.
Kwa upande wa mchezo wa kuvutana kwa kamba kwa wanaume na matokeo yakiwa kwenye mabano ni Wizara ya Elimu vs Wizara ya Mifugo (1-0); Wizara ya Ardhi vs RAS Lindi (2-0);RAS Iringa vs Wizara ya Viwanda na Biashara (2-0); Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji vs Ofisi ya Mashtaka ya Taifa (2-0); Waziri Mkuu Sera vs Ofisi ya Bunge (2-0); Wizara ya Maji vs RAS Simiyu (2-0);Ofisi ya Rais Ikulu vs Wizara ya Madini (2-0); Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) vs RAS Singida (1-0).
Katika mechi nyingine kwa wanaume Wizara ya Mambo ya Ndani vs Wizara ya Ujenzi (2-0); Wizara ya Uchukuzi vs Wizara ya Maliasili na Utalii (2-0); Mahakama vs Tume ya Maadili (2-0); Wizara ya Afya vs RAS Shinyanga (2-0); Hazina vs Ofisi ya Wakili Mkuu (2-0) na Haki vs Tume ya Sheria (1-0). Wakati kwa upande wa wanawake Wizara ya Mambo ya Ndani vs Maliasili na Utalii (1-0); RAS Geita vs Uwekezaji (2-0); Hazina vs Wizara ya Kilimo (2-0); Wizara ya Mambo ya Nje vs RAS Shinyanga (2-0); Ofisi ya Waziri Sera vs Wizara ya Viwanda na Biashara (2-0).
Mechi nyingine za wanawake ni Tume ya Sheria vs RAS Singida (2-0);Wizara ya Mifugo na Uvuvi vs Ofisi ya Wakili Mkuu (2-0); Ofisi ya Mashtaka ya Taifa vs RAS Kilimanjaro (2-0); Mahakama vs Katiba na Sheria (2-0); Haki vs Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (2-0); Ofisi ya Bunge vs Wizara ya Ardhi (2-0); Wizara ya Uchukuzi vs Wizara ya Maji (2-0); TAMISEMI vs Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi (2-0); Wizara ya Afya vs Wizara ya Ujenzi (2-0) na RAS Tanga vs RAS Simiyu (2-0).
Michezo hiyo inaendelea kesho kwenye viwanja vya Jamhuri, Shule ya Sekondari ya Morogoro, Chuo cha Ujenzi, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kampasi Kuu na Mazimbu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment