Nafasi Ya Matangazo

August 06, 2024


Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania George Mandepo akisaini Kitabu cha Wageni.


Maafisa wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakimpatia maelezo kuhusu namna ya kazi ya kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda hiyo inavyofanyika.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania George Mandepo akiingia kwenye banda la Tume hiyo lililopo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Nane nane yanayofanyika kwenye Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
***********
Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania imewasisitiza Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni mbalimbali kuhusu sheria ambazo wanaona zinamapungufu na zinahitaji marekebisho ili tume hiyo iweze kuzipitia na kuzifanyia tafiti kwa ajili ya kuzirekebisha kabla ya mapendekezo hayo kupelekwa  Serikalini. 

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania George Mandepo, (6 Agosti, 2024) mara baada ya kutembelea banda la Tume hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Mandego amesema wajibu mkubwa wa Tume hiyo ni kupendekeza marekebisho ya sheria, kufutwa kwa sheria au kuboresha mifumo ya usimamizi wa sheria ambazo zipo Serikalini ili ziweze kutenda haki kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. 

“Tume kabla ya kurekebisha sheria inafanya utafiti kwa uhakika kuhusu sheria husika kwa kuangalia mazingira ya sasa na mazingira yajayo kwa sababu sheria inaishi”, Amesisitiza Mandego.

Katibu Mtendaji huyo wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania amesema pamoja na Tume kufanya mapitio ya sheria na kuzirekebisha pia ina wajibu wa kuangalia iwapo sheria inayotungwa kama inaweza inaweza kuleta madhara ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Ameeleza kuwa mchakato mzima kwa kurekebisha sheria inashirikisha kikamilifu wadau wa sekta husika ikiwemo wananchi ili kuhakikisha sheria inayotungwa inakuwa bora kwa ajili ya maslahi ya mapana ya pande zote Mbili. 
Posted by MROKI On Tuesday, August 06, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo