Nafasi Ya Matangazo

August 07, 2024












Mjiolojia kutoka Tume ya Madini, Patrick Machumu ametoa elimu hiyo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chibelele iliyopo Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, leo Agosti 7, 2024 katika Banda la Tume ya Madini kwenye Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ambapo amesema, Madini aina ya Anyolite yanatokana na neno la Kimasai lenye maana ya Kijani. Madini hayo yanapatikana eneo la Mundarara Wilayani Longido mkoani Arusha.

Machumu amesema  kuwa, mwamba huo una sifa kubwa  kwa sababu ya uwezo wake wa kubeba madini ya Rubi (Ruby in Zoisite) ambayo ni miongoni mwa madini yenye thamani kubwa sokoni. Pia unaweza kutumika kutengeneza vito na urembo mbalimbali.

Amesema pia yapo madini ya Quartz ambayo  yanatumika kwa ajili ya kutengeneza vito lakini pia yanaweza kutumika kama madini ya viwandani kwa maana ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo, glasi za kutumia majumbani na vioo. 

“Kuna madini pia ya Gypsum (Jasi), haya ni madini ya viwandani  ambayo yanatumika kutengeneza bidhaa mbali mbali ikiwemo Gypsum board zinazotumika kama ceiling board majumbani, inatumika kama kiungo kwenye uzalishaji wa saruji, vile vile inatumika kama kiungo mahususi kwenye kutengeneza mbolea kwa ajili ya wakulima wa mazao tofauti tofauti,”amesema Machumu.

Aidha, amesema madini ya Magnesite ni ya viwandani na  yanatumika kama kiungo wakati wa kutengeneza mbolea na saruji, vile vile yanatumika kutengeneza vyungu vya kuchomea sampuli za dhahabu (Crucibles).

Kwa upande wa mwanafunzi Noadia Nollo wa Kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Chibelela  akizungumza kwa niaba ya wenzake mara baada ya kupewa elimu hiyo, amesema wamefahamu umuhimu wa madini, kazi za madini, aina ya  madini ambayo ni ya viwanda na vito.

Nae, Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Dodoma, Joseph Chitinka akizungumza mara baada ya kupewa elimu ya mawe na leseni amesema atawahamasisha wana ushirika kujiunga ushirika madini.

“Nimefika  kwenye banda la Tume kupata elimu, tunao ushirika wa madini na Dodoma ni miongoni mwa mikoa yenye madini mengi,  tumejifunza namna ya kuchakata na kupata leseni za uchimbaji mdogo wa madini (primary mining license ) tuna sera na kanuni zetu ambazo wakipata leseni itakuwa ni utambulisho wao tunaenda kuhamasisha watu ili waweze kujiunga na chama cha ushirika wa madini  ili kuwekeza kwenye Sekta ya Madini,”amesema Chitinka.
Posted by MROKI On Wednesday, August 07, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo