Kwenye mitandao ya kijamii inaonekana video
inayosambazwa ikimwonyesha binti anayesemekana ametokea Yombo Dovya Jiji la Dar es Salaam
akidhalilishwa na kufanyiwa ukatili ambao haukubaliki kwani ni kinyume cha
sheria, maadili ya Mtanzania na
Haki za Binadamu.
Tunapenda kutoa taarifa kuwa, Jeshi la Polisi limeshaanza kulifanyia kazi tukio
hilo ovu na la kulaaniwa.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Wananchi wote waache kuendelea
kusambaza video hiyo kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria lakini pia ni
kitendo cha kuendelea kudhalilisha utu wa
binadamu mwenzetu.
Pia tunatoa wito kwa mwenye taarifa ya kuhakikisha mkono wa sheria
unawafikia kwa haraka waliofanya ukatili huu asisite kutusaidia kwa kutupa
taarifa au kumpatia kiongozi yeyote yule wanayemwamini kwamba taarifa ikimfikia
watu hao watapatikana haraka iwezekanavyo au toa taarifa kupitia namba hii 0699
99 88 99.
Imetolewa na:
David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma,Tanzania
0 comments:
Post a Comment