Nafasi Ya Matangazo

August 30, 2024













Tafiti za kidemografia mwaka 2022 zinaonesha kuwa utekelezaji wa afua za lishe kwa Mkoa wa Dodoma unaendelea kuimarika kwani hali ya udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano imeshuka kutoka 37% (2015 -2016) hadi 30.

Akitoa hotuba ya ufunguzi katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa lishe kwa Julai-2023 hadi Juni 2024 kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi yake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule ambaye ndiye Mwenyekiti wa kikao hicho, amesema;

“Tafiti hizi zinaonesha kuwa Mkoa umeimarika kwenye suala la lishe ingawa tafsiri yake ni kwamba katika watoto 100, watoto 30 wana udumavu. Hali hii sio nzuri kwa Mkoa na Taifa kwa ujumla ingawa hali ya utekelezaji wa Afua za lishe kwa Mkataba huu inaendelea kuimarika” Amesema Mhe. Senyamule.

Hata hivyo, kupitia kikao hicho, Mkuu wa Mkoa huyo ameongelea tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Mpox ambao umeathiri watu kadhaa kutoka mataifa jirani hivyo Mkoa wa Dodoma nao unachukua tahadhari.

“Serikali kupitia Wizara ya afya imetoa taarifa kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Mpox katika nchi zinazotuzunguka. Ugonjwa huu unasababishwa na virusi, tunamshukuru Mungu nchi yetu ipo salama na hakuna taarifa ya uwepo wa mgonjwa”

Aidha, ametaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni upele, malengelenge au vidonda kwenye mwili hasa mikononi, miguuni, kifuani, usoni na wakati mwingine hata sehemu za siri, homa, maumivu ya kichwa, misuli, mgongo, uchovu na kuvimba mtoki ambapo amewata wananchi kuchukua tahadhari zote zinazoelekezwa na watalamu wa afya.

Kadhalika Katibu tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya, amesisitiza suala la upandaji miti ya matunda kwa wanafunzi kwa kipindi cha miaka wanayokaa shuleni kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha lishe kwa kupata uhakika wa matunda ya kutosha.

Katika hatua nyingine, Mkoa umetoa zawadi ya vyeti vya pongezi kwa Halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma kwa kufanikiwa kutekeleza viashiria vyote vya lishe vilivyopo kwenye Mkataba kwa asilimia 98. Hii inaashiria kuwa Mkoa wa Dodoma unapiga hatua kwenye suala la lishe.               
Posted by MROKI On Friday, August 30, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo