Nafasi Ya Matangazo

July 09, 2024







Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  imetakiwa kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mbegu za miche ya miti ili zifikie  wananchi wengi zaidi na hatimaye kushiriki katika kuongoa misitu iliyotoweka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) wakati wa ziara ya kikazi katika Kituo cha Uzalishaji mbegu za Miti leo Julai 9,2024  Mkoani Morogoro.

"Tuendelee kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mbegu na vyanzo vya mbegu na pia tuongeze Bajeti kukiwezesha kituo hiki" Mhe. Kairuki amesema.

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki amewataka kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na wahariri ili jamii ifahamu umuhimu wa mbegu bora za miti.

"Ni lazima muwe na maabara ya kisasa na pia mkitangaze kituo hiki kijulikane tuna mbegu za miche aina gani na tuna maabara" ameongeza.

Aidha, Mhe Kairuki ametilia mkazo suala la ukusanyaji maduhuli kujifanyia tahmini katika makusanyo na wanachotoa kwa Serikali.

Amewataka kutafuta  ushirikiano katika Taasisi nyingine Duniani kupitia  balozi  zilizopo nchini  lengo ikiwa ni kuongeza tija na mapato ya kituo hicho.

Kituo cha uzalishaji mbegu za Miti kiko chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ambapo kinazalisha mbegu za miche ya matunda ya muda mfupi, miche ya mbao,kuni,kivuli, mapambo na miti ya kilimo mseto.
Posted by MROKI On Tuesday, July 09, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo