Nafasi Ya Matangazo

July 10, 2024

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Godfrey Mnzava akimpatia kitambulisho cha bima ya Afya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Darajani wilayani Mkalama.

Godfrey Mnzava - Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru akizungumza wakati wa kutoa ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wananchi wa wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Matukio mbalimbali ya picha katika mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Makalama
Mwonekano wa Bweni la Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum katika shule ya msingi Darajani ambalo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru amekataa kulizindua kutokana na Kuchunguzwa na Takukuru.
Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kati ya Mkuu wa wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda na Mkuu wa wilaya ya Mkalama Moses Machari.
***************
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Godfrey Mnzava amekataa kuweka jiwe la msingi katika bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Darajani wilayani Mkalama baada ya kubaini kuwa ujenzi wa bweni hilo na uzio unachunguzwa na Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa -Takukuru- wilaya ya Mkalama.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa uhuru amemwagiza Mkuu wa Takukuru wilaya ya Mkalama kumpatia taarifa ya awali ya uchunguzi hapo kesho ili waweze kujiridhisha kuhusu uchunguzi unaofanywa kwa sasa na Taasisi hiyo.
Ujenzi huo wa Bweni la Wanafunzi wenye Mahitaji maalum katika shule ya msingi Darajani wilayani Mkalama umegharimu zaidi ya shilingi milioni 140.

Mnzava pia amewataka Watendaji wa Halmashauri ya Mkalama kumpatia taarifa kuhusu mchakato wa ukataji wa bima za afya kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwenye shule ya msingi darajani ili kujua kama kwenye kama gharama za kuwakatia bima wanafunzi hao zimefuata taratibu.

Akiwa katika shule ya Sekondari ya Mkalama One, Kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa Uhuru ametoa muda wa siku Saba kuanzia sasa kupatiwa taarifa kuhusu kwa nini ujenzi wa shule hiyo ya Sekondari ya Mkalama haujakamilika licha ya Serikali kutoa zaidi ya shilingi milioni 544.

Amesisitiza kuwa nia ya Serikali ya kujenga shule za msingi na Sekondari nchini ni kusogeza huduma karibu na wananchi hivyo ni muhimu kwa Watendaji kusimamia miradi hiyo kikamilifu kulingana na thamani ya fedha na sio vinginevyo.

Awali akitoa taarifa kuhusu miradi ya maendeleo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru, Mkuu wa wilaya ya Iramba Moses Machari amesema mwenge huo wa uhuru utatembelea,kukagua, kuweka mawe ya msingi pamoja na kuzindua miradi ya maendeleo Saba yenye Thamani ya zaidi ya shilingi bilioni Mbili.
Posted by MROKI On Wednesday, July 10, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo