Nafasi Ya Matangazo

June 21, 2024

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumuaga Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani aliyemaliza muda wake Mhe. Jumanne Sagini (Mb) Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na kumkaribisha Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Mhe. Daniel Sillo (Mb) ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi iliyofanyika katika Hoteli ya Morena Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama (NUU) pamoja na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walishiriki hafla hiyo fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Morena Jijini Dodoma.
Wenyeviti wa Kamati za Usalama Barabarani nchini wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani aliyemaliza muda wake Mhe. Jumanne Sagini (Mb) Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na kumkaribisha Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Mhe. Daniel Sillo (Mb) ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi iliyofanyika katika Hoteli ya Morena Jijini Dodoma. _*(Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)*_
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu (kushoto), akimkabidhi Tuzo ya Heshima Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani aliyemaliza muda wake Mhe. Jumanne Sagini (Mb) Naibu Waziri wa Katiba na Sheria (kulia) iliyotolewa na Wenyeviti wa Kamati za Usalama Barabarani Tanzania wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Morena Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu (Aliyevaa kofia), akimkabidhi Zawadi Mwenyekitiki mpya wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo (Mb) (kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Morena Jijini Dodoma.
**************
Na Mwandishi wetu
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu, ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutafuta mwarobaini utakaopelekea kupunguza matumizi ya pombe aina ya (sungura) zisizo na vipimo kwa baadhi ya madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda kwani ndio chanzo cha ajali za barabarani.

Akizungumza alipokuwa Mgeni Rasmi katika hafla fupi ya kumuaga Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani aliyemaliza muda wake Mhe. Jumanne Sagini (Mb) Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na kumkaribisha Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Mhe. Daniel Sillo (Mb) ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi iliyofanyika katika Hoteli ya Morena Jijini Dodoma alisema waathirika wakubwa wa ajali za bodaboda ni vijana kutokana na unywaji wa pombe wakiwa barabarani.

"Taifa limepoteza nguvu kazi kutokana na ajali za bodaboda ambazo zinasababishwa na unywaji wa pombe za gharama za chini ukienda MOI Serikali inatibu vijana ambao wengi wao ni ajali za bodaboda hivyo naombeni msimamie katika kupunguza ajali na kutoa elimu pia sina budi kumpongeza Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani aliyemaliza muda wake Mhe. Jumanne Sagini kwani sisi sote ni mashahidi kuwa juhudi zake za kupambana na ajali zimeonekana" Alisema Mhe. Zungu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani aliyemaliza muda wake ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini alimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni kwa usimamizi mzuri na ushirikiano mkubwa alioutoa kwa kipindi chote ambacho akiwa mwenyekiti.

Pia Mhe. Sagini alisema kuwa mafanikio yaliyopatikana katika uongozi wake ni Juhudi za wenyeviti na viongozi wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kwani hawakuwa nyuma na yote mazuri yaliofanyika ni ushirikiano wao wote kutokana na timu nzuri iliyoundwa ya ushindi na bado ipo inaendelea.

Kwa upande wake Mwenyekitiki mpya wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo aliwashukuru wenyeviti wanaunda Baraza hilo kwa kumkaribisha vyema ambapo aliwahakikishia kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mhe. Jumanne Sagini.

Aidha, alimpongeza Naibu Spika kwa kukubali Wito wa kushikiriki kama mgeni rasmi katika hafla hiyo ambapo alimhakikishia kuwa katika Bajeti ya Serikali ya 2024/2025 tayari Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeanza mchakato wa kununua vifaa vya kudhibiti ajali zikiwemo kamera ambazo zitafungwa baadhi ya miji na mitambo ya kisasa ya kukagua vyombo vya moto barabarani.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama (NUU) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mhe. Vita Kawawa (Mb), pamoja na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Posted by MROKI On Friday, June 21, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo