Nafasi Ya Matangazo

June 23, 2024

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI), wamekutana leo kwenye kikao cha kupanga tarehe za bonanza la uzinduzi na michezo ya SHIMIWI mwaka 2024 kilichofanyika Jijini Dodoma.
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI),  wakiwa katika picha ya pamoja leo baada ya kumalizika kwa kikao cha kupanga tarehe za bonanza la uzinduzi na michezo ya SHIMIWI mwaka 2024 kilichofanyika Jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI), Bw. Alex Temba (kulia) akipokea rambirambi kutoka kwa viongozi na wanamichezo wa shirikisho hilo iliyokabidhiwa na Mwenyekiti Bw. Daniel Mwalusamba (wapili kulia) baada ya kufiwa na mama yake mzazi hivi karibu. Wanaoshuhudia wa pili kushoto ni Bw. Michael Masubo (Makamu Mwenyekiti) na kushoto ni Mjumbe Bi. Itika Mwankenja.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw. Daniel Mwalusamba (wapili kushoto) leo amemkabidhi Bw. Apollo Kayungi (wapili kulia) fedha za rambirambi zilizochangwa na viongozi na wanamichezo wa michezo hiyo kufuatia kifo cha baba yake mzazi aliyefariki hivi karibuni. Wanaoshuhudia wa kushoto ni Bw. Michael Masubo (Makamu Mwenyekiti) na kulia ni Mjumbe Bi. Itika Mwankenja

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MAANDALIZI ya michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yameanza ambapo Kamati ya Utendaji imependekeza michuano hiyo kufanyika Septemba 2024 mkoani Morogoro.

Timu zinazoshiriki michezo hiyo zimehimizwa kufanya maandaalizi kwa watumishi wa serikali kutoka kwenye wizara, taasisi, wakala za serikali, ofisi za wakuu wa mikoa na halmashauri na manispaa ili kushiriki bonanza la uzinduzi litakalofanyika Agosti jijini Dodoma na hatimaye michuano ya SHIMIWI mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa SHIMIWI, Alex Temba amesema mgeni rasmi wa bonanza hilo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka ambaye ni mlezi wa Shirikisho hilo.

Temba amesema michezo itakayofanyika kwenye bonanza hilo litakalofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma ni pamoja na kuvuta kamba kwa wanawake na wanaume, mpira wa miguu, netiboli na mbio za watu wazima wenye umri wa kuanzia miaka 55

“Tarehe rasmi ya michezo yetu pamoja na hili bonanza kubwa itatangazwa baadaye mwezi huu maana ni utaratibu wetu lazima michezo itanguliwe na bonanza kubwa lenye kushirikisha watumishi wa umma wenye kushiriki kwenye michezo hii ya SHIMIWI,” amesema Temba.

Hata hivyo, amezitaka timu kuanza kuandaa timu zao kwa ajili ya kushiriki kwenye bonanza hilo, ambapo amesema rekodi inaonesha ushiriki wa klabu kwenye michezo hii unaendelea kuongezeka kutoka 47 kwa mwaka 2021 na kufikia 62 ilikuwa mwaka 2022, na 2023 kulikuwa na klabu 74.

Kikao hicho kimeudhuriwa pia na Mwenyekiti wa SHIMIWI, Bw. Daniel Mwalusamba ambaye awali alitoa wito kwa timu kuanza maandalizi ya michezo ya SHIMIWI, ili kuleta ushindani bora kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

Mwalusamba amesema kwa kuwa mwaka huu michezo itatanguliwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa, ametoa wito kwa watumishi kuelekeza akili zao pia katika maelekezo ya watendaji wakuu wa serikali kuhusiana na uchaguzi huu.
Posted by MROKI On Sunday, June 23, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo