Nafasi Ya Matangazo

June 06, 2024








Na Mwanahamisi Msangi, Songwe
TUME ya Madini Mkoa wa Songwe  imeunda kikosi kazi maalum cha kupambana na kudhibiti utoroshaji  wa madini na kusababisha serikali kukosa mapato.

Hayo yamesemwa na Afisa Madini Mkazi - Songwe, Chone Malembo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatembelea wachimbaji wadogo katika eneo la Mbangala lililopo mkoani humo.

“Kwa sasa kuna mawasiliano ambayo yanaendelea tunataka kutengeneza kikosi kazi madini Mkoa ambacho kazi yake itakuwa ni kufanya uchunguzi  na kutoa taarifa kuhusu utoroshaji madini mahali husika ili kuchukua hatua stahiki lengo ni kudhibiti utoroshaji ambao husababisha Serikali kukosa mapato,”amesema Chone.

Katika hatua nyingine, Afisa huyo amesema wamegundua madini mapya aina ya Solidite ambayo yanapatikana Wilaya ya Momba.
Posted by MROKI On Thursday, June 06, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo