Nafasi Ya Matangazo

June 05, 2024

Wananchi wa Jiji la Dodoma na viunga vyake wameendelea kujitokeza katika Kliniki ya Ardhi ili kutatuliwa migogoro ya ardhi inayowakabili.

Kamishna wa Ardhi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Methew Nhonge amesema Watendaji wakuu wa Wizara pamoja na watendaji wa Ardhi mkoa wa Dodoma wapo katika eneo la Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kutoa huduma kwa wananchi wanaofika eneo hilo kupata huduma za ardhi.

Kwa kipindi cha siku mbili tangu Juni 3-4, 2024 jumla ya wanaanchi 996 wamefika katika viwanja hivyo na kupatiwa huduma kulingana na mahitaji yao.

Watendaji hao wamepiga kambi katika Ofisi hizo kwa lengo la kutekeleza agizo la Mhe. Jerry Silaa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alilolitoa Bungeni Mei 27, 2024 la kuhamisha Masijala ya Ardhi kutoka jiji la Dodoma na kuzihamishia katika Ofisi za Wizara ili kutatua migogoro ya ardhi katika kituo kimoja jumuishi (One Stop Center).
Posted by MROKI On Wednesday, June 05, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo