Nafasi Ya Matangazo

May 15, 2024




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar na Comoro zina Mahusiano maalum ya kuchanganya damu wa kindugu hivyo ameridhia kufunguliwa kwa Konseli Mkuu wa Comoro hapa Zanzibar. 

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Comoro Mhe.Saidi Yakubu aliyefika kumuaga baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Ikulu Zanzibar tarehe 14 Mei 2024. 

Rais Dk.Mwinyi  pia amemtaka Balozi Yakubu kuangalia fursa zilizopo za kuuza bidhaa mbalimbali kutoka nchini na kuzisimamia hati za makubaliano  ya pamoja  na kamati ya ushirikiano wa kudumu ikiwemo  katika sekta ya afya,  elimu, utamaduni, biashara, usafirishaji na  habari kupitia shirika la utangazaji Zanzibar (ZBC).

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Shirika la Meli la Zanzibar lina mpango wa kuagiza meli mbili mpya, ameleeza pia MV.Mapinduzi imeshafanyiwa ukarabati na hivi karibuni itaanza  safari zake kutoka Zanzibar kwenda Comoro.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amebainisha kuwa Zanzibar imejipanga kwa utalii wa matibabu kwa kuifanya hospitali mpya ya Lumumba kuwa kituo cha kupokea wagonjwa kutoka nje hasa nchi ya Comoro pindi itakapokamilika na kuanza kutoa huduma.

Naye Balozi Yakubu amemuahidi Rais Dk.Mwinyi kudumisha uhusiano wa kindugu uliopo kati ya Zanzibar na Comoro pamoja na kuendeleza hati za  makubaliano ya  pamoja na kamati ya ushirikiano ya kudumu.
Posted by MROKI On Wednesday, May 15, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo