Nafasi Ya Matangazo

May 06, 2024

Kamanda wa Polisi wa mkoa we Singida Amon Kakwale akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo leo.






Watuhumiwa 225 wa Makosa mbalimbali ya Uhalifu ikiwemo usafirishaji na uuzaji we Dawa za kulevya wamekamatwa mkoani Singida katika kipindi cha February hadi April mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Singida,Kamanda wa Polisi wa mkoa we Singida Amon Kakwale amesema kati ya watuhumiwa hao watuhumiwa 135 ni wa Dawa za kulevya aina ya bangi na watuhumiwa 3 wamekamatwa kwa kuhujumu miundombinu ya Shirika la Ugavi wa Umeme -TANESCO- mkoa wa Singida ikiwemo wizi wa Transfoma.

Kamanda Kakwale amesema baadhi ya kesi upelelezi unaendelea na watuhumiwa wengine wameshafikishwa Mahakamani kwa ajili ya taratibu za kisheria baada ya upelelezi wa kesi zao kukamilika.

Kamanda huyo pia amewasisitiza wananchi wa mkoa wa Singida kuendelea kutoa taarifa za siri kwa jeshi hilo ambazo zitasaidia kukamatwa kwa wahalifu Kama hatua ya kukomesha vitendo vya uhalifu mkoani Singida.
Posted by MROKI On Monday, May 06, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo