Nafasi Ya Matangazo

May 06, 2024

Mwanachuo wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anayesomea Biashara upande wa Masoko George Temba akimkabdhi zawadi za watoto waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Afisa Muuguzi Msaidizi Grace Sanga. Wanachuo hao wa UDSM walitembelea JKCI hivi karibuni kwaajili ya kutoa zawadi kwa watoto pamoja na kuchangia damu.
Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wanaosomea Biashara upande wa Masoko wakichangia damu kwaajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Wanachuo hao walichangia chupa 14 za  damu pamoja na kutoa zawadi kwa watoto waliolazwa katika taasisi hiyo.
Daktari wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joseph Mwalongo akiwaeleza wanafunzi wanaosomea Biashara upande wa Masoko kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) kuhusu magonjwa ya moyo kwa watoto wakati wanafunzi hao walipotembelea JKCI hivi karibuni kwaajili ya kutoa zawadi kwa watoto waliolazwa katika Taasisi hiyo pamoja na kuchangia damu.
Posted by MROKI On Monday, May 06, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo