Nafasi Ya Matangazo

May 08, 2024

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)  akieleza umuhimu wa ushirikiano katika maendeleo wakati wa mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania Bw. Claver Serumaga (hayupo pichani) katika Ofisi ya Waziri wa Fedha Treasure Square, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiongoza mkutano kati yake na ujumbe Benki ya NCBA Tanzania ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo nchini Tanzania, Bw. Claver Serumaga (wa tatu kulia), ulioangazia ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo, uliofanyika katika Ofisi ya Waziri wa Fedha Treasure Square, jijini Dodoma.
Mkuu wa masuala ya Biashara wa Benki ya NCBA Tanzania, Bw. Godson Biyengo, akieleza mpango wa maendeleo wa Benki yake wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania Bw. Claver Serumaga (kushoto), ulioangazia ushirikiano wa maendeleo, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha Treasure Square, jijini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa masuala ya sekta ya umma wa Benki hiyo, Bi. Judy Mkama.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (kulia), akifafanua jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania Bw. Claver Serumaga (hawapo pichani), ulioangazia ushirikiano wa maendeleo, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha Treasure Square, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania Bw. Claver Serumaga, akieleza utayari wa Benki yake wa kuongeza ushirikiano katika nyanja za maendeleo wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) uliofanyika katika Ofisi ya Waziri wa Fedha Treasure Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto) akizungumza jambo wakati wa mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania Bw. Claver Serumaga, ulioangazia ushirikiano wa maendeleo, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha Treasure Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania, Bw. Claver Serumaga (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa masuala ya Biashara wa Benki hiyo, Bw. Godson Biyengo (kushoto) na Mkuu wa masuala ya sekta ya umma wa Benki hiyo, Bi. Judy Mkama, baada ya kumalizika kwa mkutano ulioangazia ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo uliofanyika katika ofisi ya Waziri wa Fedha Treasure Square, jijini Dodoma.
Posted by MROKI On Wednesday, May 08, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo