Nafasi Ya Matangazo

April 17, 2024

Mkuu wa mkoa wa SINGIDA Halima Dendego akizungumza na Viongozi wa Serikali na Dini katika ngazi zote kuhusiana na kampeni ya kuhamasisha wazazi kuwapeleka wasichana wenye umri kati ya miaka 9 hadi 14 kwenda kupata chanjo ya mlango wa uzazi ili kuwaepusha kupata saratani.Mkuu wa mkoa wa SINGIDA Halima Dendego amewahimiza Viongozi wa Serikali na wa Dini katika ngazi zote kuanza kampeni ya kuhamasisha wazazi kuwapeleka wasichana wenye umri wa kati ya miaka 9 hadi 14 kwenda kupata chanjo ya mlango wa uzazi ili kuwaepusha kupata saratani hiyo ambayo imekuwa ikileta madhara makubwa katika kundi hilo.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida ametoa kauli hiyo kwenye kikao kilichojumuisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Viongozi wa Dini, Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na Wataalamu wa Afya kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Singida.

Naye,Mratibu wa Huduma za Chanjo Mkoa wa Singida, Jadili Mhanginoma, amesema Mkoa wa SINGIDA unatarajia kutoa chanjo hiyo kwa wasichana 178,114 wenye umri kati ya miaka 9 hadi 14 kuanzia Aprili 22 hadi 26 na kuendelea hadi Desemba mwaka huu.

Ameeleza kuwa kwa sasa tayari dozi 191,040 zimeshapokelewa na kusambazwa kwenye ngazi ya halmashauri mkoani SINGIDA.

Kwa Tanzania chanjo ya Mlango wa Uzazi -HPV-  iliidhinishwa kuanza kutumika na Shirika la Afya Duniani kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba – TMDA – mwaka 2014 ambapo kwa mkoa wa SINGIDA chanjo hiyo ilianza kutumika mwaka 2018.

Posted by MROKI On Wednesday, April 17, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo