Nafasi Ya Matangazo

April 29, 2024






Na Issa Mwadangala
Mkuu wa Mkoa Songwe Daniel Chongolo amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Ileje kupitia vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi uliopo Wilayani humo ambao una vipenyo vingi vinavyotumika kupitisha magendo.

Aliyasema hayo Aprili 28, 2024 alipokuwa na Kamati ya Usalama Mkoa baada ya kutembelea na kufanya ukaguzi katika kituo cha folodha mpaka wa Isongole.

“Kazi ya ulinzi wa nchi ni yetu sote hivyo kila mmoja wetu anapaswa kuwa makini kwa kila kitu kinachoingizwa hapa nchini na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ilizifanyiwe kazi kwa haraka na hatua za kisheria zichukuliwe”alisema Chongolo

Nae, Afisa Manadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gallus Hyera alieleza kuwa hali ya ulinzi na usalama imeimalika katika mpaka huo kutokana na operesheni na doria zinazofanyika mara kwa mara ili kuwabaini wanaovusha mangendo mpakani hapo na kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo ili jamii ichukie na kuogopa uhalifu na tabia ya uvushaji wa magendo na utoroshaji wa mbolea za ruzuku.
Posted by MROKI On Monday, April 29, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo