Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, imeendelea Wilayani Kondoa April 3/ 2024 ambapo amefanya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani humo ikiwemo Ujenzi wa Wodi ya wazazi, jengo la Mochwari na jengo la upasuaji katika hospitali ya wilaya ya kondoa.
Aidha amekagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya wasichana Kondoa pamoja ukaguzi wa nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya kondoa mji ambapo ujenzi unaendelea na unatarajia kukamilika muda wowote kwani umefika hatua za umaliziaji ( Finishing).
Hatahivyo Mhe. Senyamule ameendelea kuwahimiza watumishi wa sekta ya afya kuendelea kutunza mazingira yanayozunguka katika vituo vyao ili kuendelea kuweka mazingira safi na ya kuvutia siku zote ikiwemo kupanda miti kwa mpangilio unaofaa.
0 comments:
Post a Comment