Kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari
kumechangia mafuriko ya mara kwa mara yanayoikumba mikoa ya pwani na hivyo
kusababisha mmomonyoko wa udongo na upotevu wa fukwe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameliarifu Bunge jijini Dodoma leo Aprili
05, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini Prof. Patrick
Ndakidemi aliyetaka kufahamu kama kuna ukweli
kina cha maji ya Bahari ya Hindi nchini kimeongezeka kutokana na mabadiliko ya
tabianchi na nini athari zake.
Dkt. Jafo
amesema kuwa kuongezeka kwa maji ya bahari kunasababishwa na kupanda kwa joto la dunia
kutokana
na kuendelea kuyeyuka kwa barafu katika maeno mbalimbali ya duniani.
Amesema kuwa utafiti na
vipimo vilivyopo maji ya Bahari ya Hindi katika pwani ya Dar es Salaam unaeleleza
kuwa maji yanaongezeka kwa wastani wa kiasi cha milimita 6 kwa
mwaka tangu mwaka 2002.
Kwa mujibu wa Waziri
Jafo, upotevu wa bioanuwai muhimu ikiwemo mikoko na nyasi bahari ambavyo ni
sehemu ya hifadhi ya mazingira ni miongoni mwa madhara ya kuongezeka kwa kina
cha bahari.
Ametaja madhara
mengine kuwa kupotea kwa ardhi na kuwaacha wananchi bila ya makazi na kushindwa
kufanya shughuli za kilimo kutokana na changamoto na changamoto ya kuongezeka
kwa kiwango cha bahari.
Waziri Dkt. Jafo
ameongeza kuwa visima vya maji baridi mbali na kuingiwa na maji ya chumvi pia
miundombinu ikiwemo barabara, gati za bandari na majengo hubomolewa na
maji hayo.
Kwa upande
mwingine Waziri Jafo Serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa
kuhifadhi mazingira kuzunguka Mlima Kilimanjaro ili kulinda barafu isipate
changamoto.
Akijibu swali la
Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Shally Raymond, Dkt. Jafo amepongeza Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kuzalisha na kugawa miche kwa jamii ambayo
inapandwa na kurejesha uoto wa asili.
0 comments:
Post a Comment