Nafasi Ya Matangazo

March 27, 2024






Juma la wadau wa Elimu Mkoa wa Dodoma limetamatika Kwa viongozi mbalimbali  wa Mkoa wa Dodoma kuzungumza na kushiriki Chakula Cha Mchana na wanafunzi wa Shule za kidato Cha Sita za Mkoa huo.

Kwa nyakati tofauti akiwa katika shule ya Sekondari ya wavulana Kongwa na Shule ya wasichana kibaigwa amewaasa wanafunzi hao wa kidato Cha sita kuendelea kudumisha nidhamu hususani katika kipindi hiki wanachojiandaa na mitihani Yao na kuachana na marafiki wasiofaa ambao watawasababishia matokeo yatakayogharimu maisha ya ndoto zao.

"Tunataka A zenye nidhamu, hapa Kuna wenzenu wamechafua jina la Shule na nyie mliopo hapa tunategemea nyie mtabadilisha sura hii ambayo sio njema Kwa Mkoa, acheni tabia ya kufata mkumbo Kwa kushawishiana mambo yasiyofaa kwasababu Kila mtu ana ndoto zake na Kila moja atarudi nyumbani kwao kivyake na usipokuwa makini utaharibu maisha yako Kwa mikono yako mwenyewe kwasababu tuu ya ushawishi usiofaa kutoka Kwa marafiki zenu.

"Lazima muamue kuachana na baadhi ya mambo na kufuata miongozo yenu na kufanya bidii Ili kujitofautisha na wengine na kukuza ufaulu wenu na kujenga dhana nzuri ya shule Bora ni lazima muwe na ufaulu Bora na Shule hii ambayo nyie ndio waanzilishi itapata sifa nzuri na sisi kama Mkoa tunayo matarajio kutoka kwenu kupitia matokeo mazuri mtakayotuletea," ameasa Senyamule

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon amewataka wanafunzi hao kuendelea  kujitunza vizuri  Kwa kujiweka bize na masomo na shughuli za kielimu Ili kuepukana na vishawishi mbalimbali vitakavyowafanya kupata ufaulu usiofaa na kujenga picha mbaya ya shule Yao.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa  Mwl. Vincent kayombo amesema Mkoa wa Dodoma unaendelea na maandalizi ya kuhakikisha Mkoa unapata matokeo mazuri katika mitihani ya kidato Cha sita inayotarajiwa kufanyika kuanzia Mei 6, Mwaka huu.

Aidha Mwl.Kayombo ameweka bayana kuwa Mkoa umefanya maandalizi ya kuhakikisha wanafunzi wa shule zenye kidato Cha 6 za Mkoa huo wanashiriki chakula Cha Mchana na viongozi mbalimbali ikiwa ni katika kuwahamasisha, kuwatoa hofu na kuwajengea ujasiri wanafunzi hao katika kuelekea mitihani Yao ya kuhitimu ngazi hiyo.
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon amewataka wanafunzi hao kuendelea  kujitunza vizuri  Kwa kujiweka bize na masomo na shughuli za kielimu ikiwemo michezo Ili kuepukana na vishawishi mbalimbali vitakavyowafanya kupata ufaulu usiofaa na kujenga picha mbaya ya shule Yao.
Posted by MROKI On Wednesday, March 27, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo