Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania
(TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta (wanne kulia), akipeana mkono na Balozi wa
Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Sherif Abdelhamid mara baada ya kumalizika kwa
mazungumzo yao yaliyohusisha mashirikiano katika sekta ya miundombinu ya
barabara na madaraja yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Sherif
Abdelhamid (kulia) akisisitiza jambo kwenye mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta (wapili kushoto),
wakati walipofanya mazungumzo yaliyohusisha mashirikiano katika sekta ya
miundombinu ya barabara na madaraja yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BALOZI
wa Misri nchini Tanzania, Sherif Abdelhamid amevutiwa na miradi itayojengwa kwa
ubia wa kati ya sekta binafsi na umma (PPP) itakayokuwa chini ya Wakala ya
Barabara Tanzania (TANROADS), imeelezwa.
Mtendaji
Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta amesema hayo jana mara baada ya
kumalizika kwa mazungumzo na Balozi huyo yaliyofanyika Makao Makuu ya TANROADS
jijini Dar es Salaam.
Mha.
Besta amesema Balozi huyo ameahidi kushiriki fursa zinazopatikana kwenye miradi
ya TANROADS na ameonesha dhamira ya makampuni ya Misri kuja kushiriki kwenye
miradi ya PPP, ikiwemo ya barabara ya kulipia ya kutoka Kibaha, Chalinze hadi
Morogoro; na Barabara za Mzunguko za Jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam Outer
Ring Roads).
Miradi
mingine ya PPP ni Daraja la Pili la Kigamboni; Barabara ya kulipia ya kutoka Morogoro
hadi Dodoma na barabara ya kutoka Igawa hadi Tunduma.
“Kama
alivyosema hizi ni mojawapo ya fursa na uzoefu wa Kimataifa unaonesha kuwa kuna
Serikali nyingi Duniani zimefanikiwa kukuza uchumi wao baada ya kushirikisha Sekta Binafsi
katika kuboresha baadhi ya huduma muhimu za kijamii zilizopaswa kutolewa na
Serikali kwa mikataba maalum, na mfano mzuri ni nchi hizo ni Vietnam, »
amesema Mha. Besta.
Mha.
Besta amesema pia katika mazungumzo yao wameweza kuainisha maeneo ya
mashirikiano katika kuendeleza sekta ya ujenzi na utaalamu wa miundombinu ya
barabara na madaraja nchini.
Amesema
wamekubaliana ni namna gani Misri wanaweza kushiriki katika kuwajengea uwezo
watalaam wa TANROADS kwa kutoa mafunzo maalum na kukubali washiriki kwenda
kutembelea Misri kwa ajili ya kujifunza zaidi kutokana na maendeleo
waliyoyapata.
‘ »Tunashukuru
pamoja na mazungumzo kuwa mafupi yenye lengo la kufahamiana na kujenga
mashirikiano, wenzetu wa Misri watakuja tena kuangalia soko la ujengaji wa
miundombinu ya barabara » ‘ amesema Mha. Besta.
Pia
amesema Balozi Abdelhamid amefurahishwa na ujenzi wa bwawa la Umeme la Mwl
Nyerere, ambalo linajengwa na Kampuni ya Arabs Contractors ya kutoka Misri.
0 comments:
Post a Comment