Nafasi Ya Matangazo

March 07, 2024

Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) Dar es Salaam Rordriguez Peter akimkabidhi zawadi ya picha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya alipomtembelea ofisini kwake Machi 06, 2024.

Mwanafunzi Rordriguezi amemtembelea Kamanda Mallya ofisini kwake kwa lengo la kumpongeza kwa juhudi za utoaji elimu kwa jamii juu ya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto.

Mwanafunzi huyo alimkabidhi Kamanda Mallya moja ya picha yake aliyopiga shule ya Msingi Queen Of Apostles iliyopo Mlowo Wilayani Mbozi mnamo Februari 22, 2024 alipokuwa anatoa elimu ya madhara ya ukatili shuleni hapo.

Kwa upande wake, Kamanda Mallya amemshukuru mwanafunzi huyo kwa zawadi hiyo na amesema  juhudi hizo zinafanywa na askari wote wa Mkoa wa Songwe na anatumaini kupitia askari hao Songwe bila ukatili itawezekana.
Posted by MROKI On Thursday, March 07, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo