Na Issa Mwadangala
Mtandao wa Askari Polisi
wanawake Mkoa wa Songe katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani Machi 8 mwaka
huu, wamemshika mkono Bi. Lenes Masebo Mkazi wa Itumba wilayani Ileje mkoani
Songwe .
Mtandao huo unaojumuisha Askari
wanawake kutoka Vikosi vya Polisi, Magereza na Uhamiaji wamemtembelea mama huyo
na kumpa msaada wa vitu mbalimbali kwa matumizi ya nyumbani.
Msaada huo umekuja kuelekea
kilele cha siku ya wanawake duniani baada ya Polisi kata wa kata hiyo Koplo
Yasinta, kugundua bibi huyo anaishi kwenye mazingira magumu na anauhitaji wa
kusaidiwa kutokana na bibi huyo kuishi na wajuuku wake wanne bila kuwa na
msaada wa mtu yeyote baada ya kufiwa na watoto wake nane kati ya 10 aliowaza ikiwa pamoja na mume wake
na kubakiwa na watoto wawili ambao nao hawana uwezo wa kumsaidia na wanaishi
nje ya Mkoa wa Songwe.
Akizungumza baada ya kukabidhi
mahita hayo Machi 06, 2024 Mkuu wa Kituo cha Polisi Vwawa, Mrakibu Msaidizi wa
Polisi (ASP) Veronica Myovela kwa niaba ya askari waliomtembelea bibi huyo
amesema kuwa ni muhimu kutoa kwa watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na
wenye uhitaji ili kuwatia moyo na kuwaleta karibu na jamii.
Naye, Bi. Lenes amelishukuru
Jeshi la Polisi kwa kumtembelea nyumbani kwake na kumpa mahitaji hayo,
"nimefurahi kwa kitendo cha Jeshi la Polisi kunitembelea na kunipa msaada
wa vitu mbalimbali, namshukuru Mungu kwa kuwaongoza Askari hawa, nawaombea kwa
Mungu aibariki kazi yao" alisema Bi Lenes.
Posted by MROKI
On Thursday, March 07, 2024
No comments
0 comments:
Post a Comment