Nafasi Ya Matangazo

March 07, 2024

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimsikiliza  Mkurugenzi wa Sayansi, Makumbusho ya Viumbe hai Berlin, Dkt. Andreas Kunkel (kushoto) akifafanua kuhusu mabaki ya mjusi mkubwa duniani aina ya “Dinosaur”yaliyohifadhiwa katika jumba la Makumbusho hayo nchini Ujerumani. 

Mjusi huyo Mkubwa Zaidi kuwahi kutokea duniani aligundulika 1907-1913 katika vilima vya Tendaguru mkoani Lindi nchini Tanzania. Mabaki ya mjuzi huyo yalipelekwa Ujerumani kati yam waka 1909-1913 na mjusi huyu anashikilia rekodi duniani (Guinness World Records) kama mjusi mkubwa zaidi duniani (urefu wa 13.27m) na usasa ni kivutio kikubwa cha utalii Ujerumani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (katikati) akimsikiliza  Mkurugenzi wa Sayansi, Makumbusho ya Viumbe hai Berlin, Dkt. Andreas Kunkel (kushoto) akifafanua kuhusu mabaki ya samaki yaliyohifadhiwa katika jumba la Makumbusho hayo nchini Ujerumani. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utali, Dkt. Thereza Mugobi.
Badhi ya Mafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake wakihudumia wageni katika banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Utalii ya ITB Berlin nchini Ujerumani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi zawadi  Rais ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Utalii Duniani (World Travel and Tourism Council-WTTC) Julia Simpson mara baada ya kikao cha kujadili namna ya kushirikiana kutangaza utalii, kilichofanyika katika banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Utalii  ya ITB jijini Berlin, Ujerumani leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na makampuni makubwa ya utalii ya nchini Ujerumani yenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania  katika kikao kilichofanyika kwenye banda la Tanzania katika Maonesho ya Utalii ya ITB jijini Berlin, Ujerumani leo.



Posted by MROKI On Thursday, March 07, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo