Stella Mwakilembe Afisa Ustawi wa Jamii katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam akipokea msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wa Saratani kutoka kwa wafanyakazi wanawake wa Benki ya Access leo Machi 8, 2024.
Wafanyakazi wanawake kutoka Benki ya Access wakishusha vifaa mbalimbali kwenye gari ambavyo vimetolewa kwa wagonjwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhi kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.
......................
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyoko Jijini Dar es salaam imepokea vifaa vya msingi ambavyo wagonjwa wanatumia ikiwemo Colostomy Bags,Pambazi za watu wazima pamoja na mahitaji ya kila siku ambayo ni Sabuni za kuogea,kufulia,miswaki dawa za meno na mahitaji mengine mengi.
Hayo yamebainishwa Leo Ijumaa Machi 8, 2024 na Afisa Ustawi wa Jamii katika Taasisi hiyo Stella Mwakilembe wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada kwa wafanyakazi wanawake wa Benki ya Access.
Amesema wagonjwa wa Saratani ni wagonjwa wanaougua muda mrefu na hivyo kupelekea kuyumba kiuchumi kwahiyo wanapoletewa vituo kama hivyo vinawasaidia kwenye mahitaji yao ya kila siku.
Mwakilembe amesema kuwa katika taasisi hiyo kunakituo cha kuchangia damu hivyo alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kufika kwaajili ya kuchangia damu kwani uhitaji ni mkubwa.
Kwaupande wake Meneja wa tawi la Benki ya Access iliyoko Kijitonyama Jijini Dar es salaam Sylvia Faustine amesema wameadhimisha siku ya wanawake Duniani kwakuwafariji wagonjwa wa Saratani walioko katika Taasisi ya Ocean Road sanjari na kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha wanawake katika nyanja mbalimbali.
"Tunatoa shukurani kwa uongozi wa Ocean Road kwakutupa nafasi ya kushiriki na watu wenye mahitaji maalum,tumeweza kuwaletea vitu ili viweze kuwasaidia wagonjwa Hawa", amesema Faustine
0 comments:
Post a Comment