Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano
wa Jukwaa la Biashara lililowahusisha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania
na Norway Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024. Viongozi,
Wawekezaji na Wafanyabiashara mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa Jukwaa la
Biashara lililowahusisha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Norway
Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.
Viongozi,
Wawekezaji na Wafanyabiashara mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa Jukwaa la
Biashara lililowahusisha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Norway
Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akichangia jambo
katika Mkutano wa Jukwaa la Biashara lililowahusisha Wafanyabiashara na
Wawekezaji wa Tanzania na Norway Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.
Viongozi,
Wawekezaji na Wafanyabiashara mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa Jukwaa la
Biashara lililowahusisha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Norway
Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.
Viongozi,
Wawekezaji na Wafanyabiashara mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa Jukwaa la
Biashara lililowahusisha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Norway
Jijini Oslo tarehe 13 Februari, 2024.
************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kwa mwaka 2024 Shirika la Fedha
Duniani (IMF) limesema
kuwa Tanzania inatarajia
kuwa
kati ya nchi 20
zenye uchumi unaokuwa kwa
kasi
duniani.
Rais Samia
amesema hiyo
ni fursa kwa wawekezaji wa Norway nchini Tanzania kwani pia ina mazingira
mazuri ya
kisiasa, kijiografia na kiuchumi.
Wakati akihutubia Mkutano wa
Jukwaa la Biashara kati ya nchi hizo mbili, uliofanyika jijini Oslo, Rais
Samia amebainisha
zipo kampuni kadhaa za Norway
zilizotumia fursa hiyo vizuri kwa uchumi wa Tanzania.
Aidha, Rais
Samia amesema kisiasa Tanzania ina amani chini ya demokrasia imara wa mfumo wa vyama vingi wenye kuzingatia tunu za utawala bora, kuheshimu haki za
binadamu na utawala wa sheria.
Kwa upande wa kijiografia, Rais Samia
amesema
Tanzania inafaa kwa uwekezaji
kwani ina Bandari ya Dar es Salaam katika Bahari ya Hindi, inayohudumia mataifa manane ya Afrika inayopakana
nayo.
Kiuchumi Tanzania ina sera nzuri na
imara za kiuchumi na kifedha huku
ukuaji wa Pato la Taifa
(GDP) ukirejea kwenye 5.2% kwa mwaka. Unatarajiwa kufikia zaidi ya 6% kwa mwaka ujao kama ilivyokuwa kabla ya
COVID 19.
Rais Samia amesisitiza fursa tano za
kipaumbele zikiwemo uwekezaji katika nishati
mbadala, kilimo, mafuta na gesi, mifuko ya uwekezaji, miundombinu na
usafirishaji.
Rais Samia
ameanza ziara ya Kitaifa nchini Norway kwa muda wa siku mbili baada ya kutoka
kwenye ziara ya Kihistoria huko Vatican ambapo alikutana na kufanya mazungumzo
na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis.
0 comments:
Post a Comment