Na
Mwandishi Wetu, Morogoro
Katika kuhakikisha miundombinu ya Barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa kilometa 66.7 inakuwa imara na salama kwa watumiaji. Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imekuja na mbinu mpya ya kujenga pango lenye upana wa mita tano na kina cha mita 4.5 katika Kijiji cha Sonje ili kuwaepusha na ajali za magari Tembo wa Mbuga ya Wanyama ya Mwalimu Nyerere ambao kila mwaka hupita kwenye eneo hilo kuelekea Hifadhi ya Udzungwa.
Akizungumza
hivi karibuni na Kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa, Kaimu Mhandisi Mkazi wa Mradi
wa barabara ya Kidatu – Ifakara kutoka TANROADS, Kitengo cha Wahandisi Washauri
(TECU), Mhandisi Marcel Kiimu amesema kitu
cha kutofautisha barabara hiyo na ujenzi wa miradi mingine ni uwepo wa pango
hilo kwa Tanzania nzima halipo sehemu
nyingine yeyote.
Amesema
TANROADS kwa kushirikiana na Mkandarasi M/s Reynolds Construction Company
kutoka Nigeria wamebuni njia hiyo baada ya kuona makundi ya Tembo yakitoka
katika Mbuga ya Mwalimu Nyerere na kwenda Hifadhi ya Udzungwa kila mwezi
Desemba hadi Februari kila mwaka, na baadaye kurudi katika mbuga hiyo
waliyotoka awali.
Amesema
katika eneo wanalopita tembo kumejengwa uzio na kuwekewa umeme wa kuwashtua ili
wasiweze kusambaa kwenye mashamba na makazi ya wananchi na kuharibu mazao au
kuleta maafa kwa wakazi hao, ambao wapo jirani na pango hilo.
Mha.
Kiimu ameeleza kuwa pango hilo linauwezo wa kupitisha tembo wanne kwa wakati
mmoja ambao watatokea upande wa pili, ambao pia wametengenezewa njia kuzunguka
mlima wa kuelekea Udzungwa.
Kabla
ya ujenzi wa pango hilo wanyama hao walikuwa wakipita katikati ya barabara na
kusababisha adha kwa watumiaji wa barabara hiyo, pia kwa wakazi wa eneo hilo
kujifungia ndani na kushindwa kuendelea na majukumu yao ya kila siku ikiwemo
biashara na kilimo kwa kuhofia kupata madhara au kuuwawa na tembo hao.
Katika kuhakikisha miundombinu ya Barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa kilometa 66.7 inakuwa imara na salama kwa watumiaji. Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imekuja na mbinu mpya ya kujenga pango lenye upana wa mita tano na kina cha mita 4.5 katika Kijiji cha Sonje ili kuwaepusha na ajali za magari Tembo wa Mbuga ya Wanyama ya Mwalimu Nyerere ambao kila mwaka hupita kwenye eneo hilo kuelekea Hifadhi ya Udzungwa.
0 comments:
Post a Comment