Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akishuhudia makabidhiano ya vifaa vya awali kati ya Makumbusho ya Taifa ya Tanzania na Makumbusho ya Sultani ya Oman, vitakavyotumika kwa ajili ya kuhifadhia mikusanyo mbalimbali iliyopo katika Makumbusho ya Tanzania leo Februari 6,2024, katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Sultani ya Oman, Mhe. Jamal bin Hassan Al Moosawi (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga (kulia) vifaa vya awali vya kuhifadhia mikusanyo mbalimbali katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam leo Februari 6, 2024.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akionyeshwa na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Sultani ya Oman, Mhe. Jamal bin Hassan Al Moosawi (kushoto) eneo la Maktaba ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania lililotengwa maalum kwa ajili ya machapisho ya Oman.
Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Sultani ya Oman, Mhe. Jamal bin Hassan Al Moosawi (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb)miongoni mwa mikusanyo ya picha itakayokuja kuwekwa kwenye ukumbi mpya wa kudumu wa kihistoria, katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam leo Februari 6, 2024.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb)(wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shaidhani (kulia), Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Sultani ya Oman, Mhe. Jamal bin Hassan Al Moosawi(wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga(wa tatu kutoka kushoto), Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni , Adelaide Salema (wa pili kutoka kulia) na Mshauri wa Masuala ya Historian na Utamaduni Oman Abdulwahab Al Busaidi (kushoto) mara baada ya kikao cha wataalamu kati ya Makumbusho ya Sultani ya Oman na Makumbusho ya Taifa la Tanzania kilichofanyika katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam leo Februari 6, 2024.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) katika kikao na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Makumbusho ya Sultani ya Oman na Makumbusho ya Taifa la Tanzania kilichofanyika leo Februari 6,2024, katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya menejimenti na watumishi wa Makumbusho ya Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) katika kikao na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Makumbusho ya Sultani ya Oman na Makumbusho ya Taifa la Tanzania kilichofanyika leo Februari 6,2024, katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya menejimenti na watumishi wa Makumbusho ya Taifa.
Ujumbe wa Wataalamu kutoka Makumbusho ya Sultani ya Oman ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Sultani ya Oman, Mhe. Jamal bin Hassan Al Moosawi (hayupo pichani) katika kikao na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) kilichofanyika leo Februari 6,2024, katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shaidhani.
*****************
Na Happiness Shayo- Dar es Salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameshuhudia makabidhiano ya vifaa vya awali kati ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania na Makumbusho ya Sultani ya Oman, vitakavyotumika kwa ajili ya kuhifadhia mikusanyo mbalimbali iliyopo katika Makumbusho ya Tanzania.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 6 Februari 6, 2024 katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta jijini Dar es Salaam.
Awali, akizungumza na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Makumbusho ya Sultani ya Oman na Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Mhe. Kairuki ameushukuru ujumbe huo kwa kuweza kuleta baadhi ya vifaa vya awali ikiwa ni mwanzo mzuri wa kutekeleza Mkataba wa Mashirikiano baina ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania na Makumbusho ya Sultani ya Oman.
Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Kairuki ameahidi pamoja na mambo mengine kuvionyesha baadhi ya vifaa vya kiutamaduni vya Sultani ya Oman katika Makumbusho ya Taifa la Tanzania ili watu waweze kujua na kujifunza utamaduni wa Oman.
Aidha, Mhe. Kairuki ametumia fursa hiyo kumshukuru Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Sultani ya Oman, Mhe. Jamal bin Hassan Al Moosawi kwa kukubali ombi maalum la ujenzi wa jengo litakalokuwa Kituo cha Kiutamaduni wa Kiswahili na Oman.
Waziri Kairuki ametoa wito kwa wataalamu wa pande zote mbili za Tanzania na Oman kuweka juhudi katika kuratibu mradi huo vizuri na kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga amesema kikao hicho kimejikita katika kuainisha maeneo ya kuweka mradi wa jengo la kiutamaduni la Kiswahili na Oman, kupitia eneo ambalo litakwenda kuboresha Onesho la Historia nchini, kupitia mikusanyo yote ambayo ina viashiria vya mashirikiano baina ya Oman na Tanzania ili kuviainisha vinahitaji uhifadhi wa aina gani, vinaweza vikaoneshwa namna gani kule Oman na nchini Tanzania.
Tanzania na Oman zilisaini Mkataba wa Makubaliano (MOU) Juni 13, 2022 na baada ya majadiliano ya muda mrefu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliwezesha kufanyika kwa mkutano wa kwanza wa pamoja baina ya Makumbusho ya Tanzania na Makumbusho ya Sultani ya Oman jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 6 hadi, 8 2023 ambao ulihitimishwa kwa kusaini makubaliano yaliyolenga katika Usimamizi wa Mikusanyo, Uhifadhi wa Mikusanyo, kufanya Tafiti, Maonesho ya pamoja na programu za uhamasishaji.
0 comments:
Post a Comment