Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary akiongoza Kikao cha Kamati ya Uendeshaji
wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia
Vijijini (EBARR) kilichoketi jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary akiongoza Kikao cha Kamati ya Uendeshaji wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) kilichoketi jijini Dodoma.Sehemu ya wajumbe wakiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) mara baada ya kumalizika kwa kikao jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uendeshaji wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) mara baada ya kumalizika kwa kikao jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak.
**********
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga amewaasa wataalamu kuendelea kuibua na kuandika miradi mingine ili kutatua changamoto za mazingira nchini.
Ametoa rai hiyo wakati wa Kikao cha Kamati ya Uendeshaji wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) kilichoketi jijini Dodoma.
Bi. Maganga ambaye ni mwenyekiti wa Kamati hiyo amesistiza umuhimu wa kusimamia miradi kwa ufanisi ili matokeo yake yaweze konekana na kuinufaisha jamii.
Halikadhalika
amewasistiza wasimamizi wa mradi kuhakikisha wanakamilisha shughuli
zilizopangwa kwa wakati ili kuepusha mradi kufika mwisho wa muda wake kabla ya
shughuli kukamilika.Bi.
Maganga ni mwenyekiti Kamati hiyo inayoundwa na Makatibu Wakuu wa Wizara sita,
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na mwakilishi wa Asasi za Kiraia
(AZAKI).
Aidha,
Kamati hiyo imekutana kwa ajili ya kupokea taarifa za utekelezaji wa mradi
pamoja mapendekezo ya bajeti na mpango wa utekelezaji kwa mwaka 2024.
Katika
kikao hicho Kamati ya Uendeshaji wa Mradi kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi
ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak kimeidhinisha
bajeti na mpango wa utekelezaji kwa mwaka 2024.
Itakumbukwa
kuwa Mradi wa EBARR unatekelezwa katika wilaya za Mpwapwa (Dodoma), (Mvomero)
Morogoro, Simanjiro (Manyara), Kishapu (Shinyanga) na kwa upande wa Zanzibar
Wilaya ya Kaskazini ‘A‘ (Mkoa wa Kaskazini – Unguja).
0 comments:
Post a Comment