Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William
Mwegoha akihutubia katika kongamano la
Kimataifa linalofadhiliwa na Serikali ya Denmark kupitia mpango wa kutumia
michango ya umati kwenye kuwezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania (C4YET)
lililofanyika Jijini Arusha.
Mratibu wa Mradi wa C4YET na Mhadhiri Mwandamizi wa
Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Nsubili Isaga akitoa maelezo ya
awali katika kongamano la Kimataifa la kupitia mpango wa
kutumia michango ya umati kwenye kuwezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania
(C4YET) lililofanyika Jijini Arusha.
Washiriki wa kongamano la Kimataifa la kupitia mpango wa kutumia michango
ya umati kwenye kuwezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania (C4YET)
wakimsikiliza mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi, kongamono hilo la siku
mbili limefanyika Jijini Arusha.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya hafla ya ufunguzi.
*************
Na Mwandishi wetu, Arusha
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe,
Profesa William Mwegoha amesema tafiti mbalimbali zinazofanywa na wanataaluma
wa chuo hicho zimelenga kuwainua vijana wa kitanzania kwa kuwapatia mitaji
kupitia uchangiaji wa umati.
Profesa Mwegoha amesema hayo Januari
24, 2023 wakati wa uzinduzi wa kongamano la Kimataifa linalofadhiliwa na
Serikali ya Denmark kupitia mpango wa kutumia michango ya umati kwenye
kuwezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania (C4YET ) lililofanyika Jijini
Arusha.
Amesema tafiti hizo zimelenga
kuangalia mbinu mbalimbali, faida kwa mlengwa na faida kwa mchangiaji ili
kuwainua vijana na wajasiriamali wadogo wadogo kupitia uchangiaji wa umati.
“Kwa chuo chetu Mzumbe ni utafiti
wenye manufaa makubwa kwasababu unachangia sana kwenye dhana ya Serikali ya
kuhakikisha wajasiriamali wadogo wanawezeshwa mitaji” amesema Prof. Mwegoha.
Amesema kupitia kongamano hilo
linalowakutanisha watalaamu kutoka vyuo mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu Mzumbe na
Chuo cha Copenhagen kutoka Denmark, watafiti watabadilishana matokeo ya utafiti
na kupata njia sahihi yakutekeleza dhana ya uchangiaji wa umati.
Profesa Mwegoha amesema mradi huo
ulianza mwaka 2019 na ni wa miaka mitano ambao umewanufaisha vijana wa maeneo
yote ya mijini na vijijini.
Naye Mratibu wa mradi huo,Dkt.
Nsubili Isaga kutoka skuli ya biashara Chuo Kikuu Mzumbe amesema mradi huo
umewainua wajasiriamali kutokana na kubuni nyenzo walizotumia za uandishi wa andiko
lililowavutia wafadhili kwaajili ya wanataaluma kusaidia tafiti na hatimaye
chuo hicho kushirikisha SIDO kwaajili ya kuwakwamua wajasiriamali vijana kwenye
mikoa mitano ambayo ni Arusha, Mwanza, Dar es Salaam, Morogoro na Mbeya.
Ameongeza kuwa jumla ya wajasiriamali 187
walipewa mafunzo hayo ambapo wajasiriamali 100 kati yao waliweza kupata mikopo
yenye riba ya asilimia 5 tu inayowawezesha wao kurejesha mikopo yao kwa wakati
na baadae vijana wengine watafikiwa zaidi ili wajiunge na majukwaa ya biashara
mitandaoni
0 comments:
Post a Comment