Waziri wa ujenzi, Innocent Bashungwa (kushoto) akipitia taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Itoni-Lusitu (km 50) kwa kiwango cha zege, wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, wakati wakikagua ujenzi wa barabara ya Itoni- Lusitu (km 50) kwa kiwango cha zege, Mkoani humo.
Na Mwandishi Wetu
Serikali imeanza kutekeleza ujenzi wa barabara ya Itoni-Lusitu (km 50) kwa kiwango cha zege, ambayo itagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 113 ili kurahisisha usafirishaji wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na madini ya Chuma cha Liganga.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya Cheil Engineering Co. Ltd wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Itoni- Lusitu (km 50) kwa kiwango cha zege, Mkoani Njombe
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya China Civil Engineering Construction (CCEC) anayejenga barabara ya Itoni- Lusitu (km 50) kwa kiwango cha zege, Mkoani Njombe.Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, wakati wakikagua ujenzi wa barabara ya Itoni- Lusitu (km 50) kwa kiwango cha zege, Mkoani humo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Njombe ambaye pia ni Mbunge wa Makambako, Mhe. Deo Sanga, akizungumza jambo kwa Mkandarasi na Mhandisi Mshauri wanaotekeleza uejnzi wa barabara ya Itoni-Lusitu (km 50) kwa kiwango cha zege, Mkoani humo.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Itoni-Lusitu (km 50) inayojengwa kwa kiwango cha zege na kugharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 113, Mkoani Njombe.Na Mwandishi Wetu
Serikali imeanza kutekeleza ujenzi wa barabara ya Itoni-Lusitu (km 50) kwa kiwango cha zege, ambayo itagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 113 ili kurahisisha usafirishaji wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na madini ya Chuma cha Liganga.
Hayo yamesemwa na Waziri
wa Ujenzi, Innocent Bashungwa Wilayani Ludewa mara baada ya kukagua barabara
hiyo pamoja na kipande cha Lusitu-Mawengi (km 50) kilichokamilika kwa kujengwa
kiwango cha zege na Wananchi tayari wameshaanza kunufaika nayo.
“Mheshimiwa Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan ana mkakati maalumu na mkoa huu wa Njombe kwa kuwa fedha
hizi zote zinawekwa hapa ili kuufungua Wilaya ya Ludewa kibiashara”, amesema Bashungwa.
Aidha, Bashungwa amesema
uwekezaji unaowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika mkoa huo utafungua
fursa ya kupitisha madini ya chuma kutoka Liganga-Mchuchuma hadi kufika Njombe
na mikoa mingine.
“Nimshukuru sana
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua mikoa ya Nyanda za Juu
Kusini kwa ujenzi wa barabara za lami na zege ili kuweza kuuruhusu uchumi
uliofungwa kwa muda mrefu kamma ilivyokuwa kwenye mradi wa liganga-mchuchuma
ulivyokaa zaidi ya miaka 40” amesisitiza Bashungwa.
Vilevile, Bashungwa
amemtaka Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara Itoni – Lusitu (km
50), Cheil Engineering Co. ltd kumsimamia kwa karibu mkandarasi China Civil
Engineering Construction Cooperation ili aweze kukamilisha mradi huo kama
mkataba unavyosema amalize Disemba 2024.
Ameongeza kuwa barabara
hiyo ni kiunganishi cha nchi za Malawi na Tanzania upande wa Nyanda za Juu Kusini
ambapo ikikamilika itachochea ukuaji wa uchumi na kuwa kiungo kizuri kati ya
mgodi wa makaa ya mawe (mchuchuma) Bandari za Dar es salaam, Tanga na Mombasa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Njombe, Anthony Mtaka amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hasan kwa
kutoa bilioni 15 kwa kulipa fidia wananchi waliopisha miradi hiyo ya mchuchuma
na liganga.
Ameeleza barabara hiyo
itaongeza pato la Taifa kutokana na shughuli za kiuchumi kama uchimbaji wa
makaa ya mawe na usafirishaji wa mazao ya misitu kutoka mikoa ya Mbeya, Njombe,
Ruvuma kwenda nchi jirani na mikoa jirani ya Tanzania.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Njombe ambaye pia ni Mbunge wa
Makambako, Mhe. Deo Sanga, amesema katika mkoa huo ilani ya CCM inatekelezwa
kwa kasi kubwa kwani mabilioni ya fedha yameelekezwa huko kuanzia barabara hiyo
bilioni 11.3 imepelekwa, na barabara ya Kibena-Lupembe (km 42) kwa bilioni 75,
Kitulo-Iniho (km 36. 3) kwa bilioni 82, Njombe-Moronga -Makete (km 117.5).
Akitoa taarifa ya mradi,
Kaimu Mkurugenzi wa Miradi kutoka TANROADS, Mhandisi Jephason Nko, amesema kuwa
maendeleo ya mradi wa ujenzi wa sehemu ya barabara ya Itoni-Lusitu umefikia
asilimia 21.6 na umeweza kutoa ajila kwa watanzania 380.
Ameongeza kuwa
wameshalipa fidia kwa wananchi 190 waliopisha mradi huo kiasi cha shilingi
bilioni 2.1 sawa na asilimia 57.24 kati ya wananchi 290 ambao barabara
imewafuata.
Barabara ya Itoni -
Lusitu ni sehemu ya utekelezaji wa barabara ya Itoni-Ludewa-Manda (km 211.4)
ambayo inajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa asilimia 100 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Disemba 2024.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi
0 comments:
Post a Comment