Akizungumza wakati wa halfa ya kupokea meli ya maakasha ya Kampuni ya Emirates Shipping Lines (ESL) iliyoanza rasmi kufanya safari za moja kwa moja kutoka Nchini China kuja Tanzania kupitia bandari ya Dar es Salaam Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi David Kihenzile amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ili kurahisisha usafirishaji na uchukuzi nchini.
“Ujio wa meli hizi zinazofanya safari za moja kwa moja kutoka nchini China hadi Tanzania ni mwendelezo wa matokeo yanayojionyesha baada ya kukamilika kwa maboresho yanayofanya na Serikalini kwenye miundombonu ya bandari nchini pongezi hizi zinatakiwa kwenda moja kwa moja kwa Uongozi shupavu wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu’ amesema Naibu Waziri Kihenzile.
Naibu Waaziri Kihenzile amesema pamoja na ongezeko hilo la shehena ujio wa meli hizo utapunguza gharama za usafirishaji kwani mzigo utapakiwa nchini China na kuja moja kwa moja nchini Tanzania hivyo kupunguza gharama za usafirishaji wa shehena hususani makasha.
Aidha, Naibu Waziri Kihenzile amechukua fursa hiyo kuilekeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha meli zote zinazotoa hudhuma kupitia bandari nchini zinapewa huduma stahiki na zenye viwango.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Mrisho Mrisho amesema baada ya maboresho makubwa yaliyohusisha ujenzi wa gati na uongezaji wa kina katika lango la kuingilia bandarini kumeiwezesha bandari kuongeza idadi ya mizigo na magari inayohudumiwa kwa wakati mmoja.
Mkurugenzi Mrisho amemuhakikshia Naibu Waziri Kihenzile kuwa kwa sasa TPA imejipanga kuhakikisha kuwa inatumia vizuri mitambo iliyonayo kutoa huduma kwa uharaka na ufanisi hususani katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli ya Emirates (ESL) Kanda ya Afrika Mashariki Nahodha Nithin Nath amesema kuanza kutoa huduma za kusafirisha mizigo moja kwa moja kutoka China hadi Tanzania kunatarajiwa kupunguza muda wa safari na usafirishaji kutoka siku arobaini na tano (45) hadi siku 22) na hivyo kufanya bei za bidhaa kuushuka.
Nahodha Nath
amesema ESL imeweka mikakati ya kuhakikisha inaanzisha safari za kusafirisha
makasha ya mizigo kutoka China kwenda bandari za Tanga, Mtwara na Zanzibar.
Meli ya Kampuni ya ESL imefanya safari yake kwa mara ya kwanza kutoka nchini China kuja Tanzania na kwa safari hiyo itaweza kushusha na kupakia makasha takribani 600 ambapo kazi hiyo inatarajiwa kufanywa ndani ya saa zisizozidi 48.
0 comments:
Post a Comment