JESHI
la Polisi Mkoani Songwe kupitia kwa Kamanda wa Polisi mkoa huo, Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP. Theopista Mallya amewaasa wamini wa Kanisa
Katoliki Parokia ya Mtakatifu Hellena, Igamba
Wilayani Mbozi Jimbo Kuu la Mbeya, kukemnea vitebndo vya rushwa.
ACP. Mallya aliyasema hayo wakati akiongoza harambee ya kuchangisha pesa kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Mapadre kwa Paroko Isaya Nyambo,Igamba Wilayani Mbozi.
ACP. Mallya aliwataka waumini hao pia kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo vilivyo kinyume na Mila na Desturi za Taifa letu,hasa vinavyosababisha ukatili dhidi ya watoto.
Kamanda Mallya katika harambee hiyo aliwezesha kuchangisha kiasi cha shilingi Milioni 3 na Laki Tano kwaajili ya kununua mbao za kupaulia jengo hilo ili kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo.
0 comments:
Post a Comment