Nafasi Ya Matangazo

September 19, 2023

 
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Pindi Chana (katikati) akimsikiliza Afisa   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Bw. Frank Kanyusi. (Kulia) punde baada ya kuwasili makao makuu ya RITA jijini Dar es Salaam ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuongoza wizara hiyo., lengo ikiwa ni kujifunza kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo. , kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi.  Pauline Gekul.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Pindi Chana (katikati) akimsikiliza Afisa   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Bw. Frank Kanyusi. (Kulia) punde baada ya kuwasili makao makuu ya RITA jijini Dar es Salaam ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuongoza wizara hiyo., lengo ikiwa ni kujifunza kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo. , kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi.  Pauline Gekul.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Pindi Chana (kushoto) akisalimiana na Naibu Kabidhi Wasii Mkuu kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Bi. Irene Lesulie (kulia) punde mara baada ya kuwasili makao makuu ya RITA jijini Dar es Salaam. ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuongoza wizara hiyo,  wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi.  Pauline Gekul, na (katikati) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi.Mary Makondo na wapili kulia ni  Afisa   Mtendaji Mkuu wa RITA, Bw. Frank Kanyusi.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Pindi Chana wapili kushoto akikabidhiwa zawadi na Naibu Kabidhi Wasii Mkuu kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Bi. Irene Lesulie (katikati) punde mara baada ya kufika makao makuu ya RITA kujifunza kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo. Ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuongoza wizara hiyo, kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi.  Pauline Gekul, na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi.Mary Makondo na wapili kulia ni  Afisa   Mtendaji Mkuu wa RITA, Bw. Frank Kanyusi.
***********
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Pindi Chana amewataka watanzania kuchangamkia fursa na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima kwenye familia na jamii kwa ujumla wake.
 
Akizungumza na menejimenti na  wafanyakazi wa RITA Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara yake kwa mara ya kwanza, mbali ya kuwapongeza  kwa huduma nzuri wanayotoa, Waziri Chana aliwakumbusha watanzania kuwa RITA ndiyo suluhisho la migogoro mingi kwenye familia na  h hawana budi kuzichangamkia ikiwemo kusajili  watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kupata vyeti vya kuzaliwa bure.
 
‘’RITA ni taasisi muhimu sana kwani ndiyo sehemu pekee inayotoa huduma muhimu zinazomgusa kila mwananchi ikiwemo kutoa vyeti vya kuzaliwa, kifo, ufilisi na usajili wa wadhamini kwa hiyo hili ni eneo muhimu ambalo linahitaji kufanyiwa kazi kwa umakini mkubwa kwani kuna kundi kubwa la watanzania wanao tegemea kupata huduma kutoka RITA,”alisema Waziri Chana.  
 
Aidha, Dkt Chana alibainisha kuwa  wakati umefika kwa RITA kama taasisi yenye dhamana kuanza  kutoa huduma kidigitali ili kuongeza tija na urahisi kwa wananchi na serikali kwa ujumla kwani kufanya hivi kutasaidia upatikanaji wa taarifa kwa haraka  na kwa wakati.
 
“Sasa tunaenda kuiunganisha mifumo yetu ya utoaji taarifa ili iweze kusomana kusudi  wananchi waweze kupata taarifa mbalimbali popote walipo pasipo kufika makao,” alisema waziri na kuwahasisha  wananchi kuwasajili watoto wote waliochini ya miaka mitano.
 
Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bi.Mary Makondo  amesema wizara imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na wakala ili kuhakikisha watanzania wanapewa elimu ya kutosha kuhusu faida za kuandaa wosia na mirasi  sambamba na kuepusha migogoro na kuwasaidia kupata haki walengwa.
 
“Wananchi wengi hawana elimu  ya kutosha kuhusu wosia na mirathi hivyo RITA ina jukumu kubwa la kuhakikisha elimu inawafikia wengi pamoja na  kuwezesha wajane na watoto ambao ndiyo waathirika wakubwa kwenye kupata mirathi,”alisema Bi. Makondo.
 
Bi. Makondo alisema migogoro mingi imekuwa ikijitokeza kwenye familia wakati wa kugawa mirathi kutokana na kutokuwepo kwa wosia kama mwongozo wa jinsi ya kuigawa mali ya marehemu kwa wahusika na matokeo yake watoto na wajane hukosa haki yao ya kurithi.
 
“Wosia unasaidia kutatua migogoro ambayo isingelijitokeza wakati wa kugawa mirathi ya marehemu na mtu kuandika wosia siyo uchuro bali ni kuweka utaratibu wa mali za muhusika na namna iliyobora yakuzigawa mali za marehemu  pindi akisha fariki dunia,”alisema Bi. Makondo.
 
Kwa upande wake, Afisa   Mtendaji Mkuu wa RITA, Bw. Frank Kanyusi alisema wakala utaendelea kutekeleza maelekezo ya wizara sambamba kufikia malengo yaliyowekwa na bodi ya wadhami.
 
 Alisema wakala wanaendelea na mpango wa usajili watoto chini ya umri wa miaka mitano na mpaka sasa umeshatekelezwa katika mikoa 24  na bado mikoa miwili  ambayo ni  Kigoma na Dar es Salaam tu.
 
“Tunategemea kutekeleza mpango huo mkoani Kigoma mwezi ujao (Oktoba) na Novemba  kwa mkoa wa Dar es Salaam,” alisema Bw. Kanyusi na kumpongeza Dkt Chana kwa kuteuliwa kuiongoza Wizara ya Sheria na Katiba.
 

Posted by MROKI On Tuesday, September 19, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo