Nafasi Ya Matangazo

September 20, 2023

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika  Viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi  ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 19 Septemba, 2023.
Viongozi pamoja na Wananchi kutoka sehemu mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mitwero Mkoani Lindi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 19 Septemba, 2023.
Viongozi pamoja na Wananchi kutoka sehemu mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mitwero Mkoani Lindi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 19 Septemba, 2023.
.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema mkoa wa Lindi unakabiliwa na changamoto kubwa ya ndovu ambao huharibu mazao na kujeruhi wananchi.
 
Rais Samia amesema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Lindi iliyopo kijiji cha Mitwero.
 
Aidha, Rais Samia amesema Serikali inapanga mkakati wa kuanza kuifanyia kazi changamoto hii na kudhibiti ndovu ili kulinda usalama wa maisha na mali za wananchi.
 
Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji inayokabili maeneo mengi nchini, Rais Samia amewataka viongozi kubuni mkakati wa kitaifa ili kutatua mgogoro huo.
 
Rais Samia pia ameweka Jiwe la Msingi mradi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa Masoko inayotarajiwa kukamilika Februari 2025 kwa gharama ya shilingi bilioni 266 na kutoa ajira zaidi ya 30,000. 
 
Vilevile, Rais Samia amezindua awamu ya kwanza ya ugawaji wa boti za kisasa ambapo jumla ya boti 160 za mkopo nafuu zitagawiwa kote nchini kwa ajili ya uvuvi na kilimo cha mwani.
 
Hali kadhalika, Rais Samia ameweka Jiwe la Msingi kwenye shule ya sekondari ya wasichana Lindi, iliyoko kijiji cha Kilangala ikiwa ni moja kati ya shule 10 zinazojengwa chini ya Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP)
Posted by MROKI On Wednesday, September 20, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo