Baadhi ya Wachezaji, Viongozi
na Mashabiki wa Klabu ya Tip top ya Manzese
jijini Dar es Salaam wakishangilia na Kikombe mara baada ya kuibuka
mabingwa wa Mashindano ya wazi ya Pooltable ya Nane nane yaliyojulikana kama
“88 Grand Open Pool Competitions 2023” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika
Hoteli ya Nefaland Manzese.Tip top ilizawadiwa Kikombe, Medali za dhahabu
pamoja na pesa taslimu shilingi laki tano(500,000/=).

Bingwa wa Mashindano ya
Pooltable ya wazi yaliyojulikana kama
“88 Grand Open Pool Competitions 2023”,upande wa Wanaume mchezaji mmoja
mmoja(Singles), Abdue Kiande akicheza dhidi ya mpinzani wake Festo
Yohana(hayupo pichani) wakati wa fainali iliyomalizika mwishoni mwa wiki katika
Hoteli ya Nefaland Manzese jijini Dar es Salaam.Kiande alishinda 7- 6 na hivyo
kuzawadiwa Kikombe Medali ya Dhahabu
pamoja na pesa taslimu shilingi laki tano(500,000/=).
Bingwa wa Mashindano ya Pooltable ya wazi Wanaume mchezaji mmoja mmoja(Singles) yaliyojulikana kama “88 Grand Open Pool Competitions 2023”, Abdue Kiande kutoka klabu ya Tiptop Manzese akifurahi na Kikombe mara baada ya kuibuka bingwa wa mashindano hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Hotel ya Nefaland Manzese jijini Dar es Salaam.Kiande alizawadiwa Kikombe, Medali ya Dhahabu pamoja na pesa taslimu shilingi laki tano(500,000/=).
Bingwa wa Mashindano ya
Pooltable ya wazi Wanawake mchezaji
mmoja mmoja(Singles) yaliyojulikana kama “88 Grand Open Pool Competitions
2023”, Jackline Tido kutoka Dodoma akifurahi na Kikombe mara baada ya kupata
ubingwa huo uliomalizika mwishoni mwa wiki katika Hotel ya Nefaland Manzese
jijini Dar es Salaam.Jackline kwa ushindi huo alizawadiwa Kikombe, Medali ya
Dhahabu pamoja na pesa taslimu shilingi laki tatu(300,000/=).

Balozi wa Mchezo wa Pooltable
na Msanii wa Nyimbo za Mashairi, Mrisho Mpoto(Mjomba) akimkabidhi Kikombe
Jackline Tido mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya Pooltable ya
Wazi upande wa Wanawake yaliyojulikana kama “88 Grand Open Pool Competitions
2023” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Nefaland Manzese jijini
Dar es Salaam.Jacline kwa ushindi huo alizawadiwa Kikombe, Medali ya Dhahabu
pamoja na pesa taslimu shilingi laki tatu(300,000/=).

Bingwa wa Mashindano ya
Pooltable ya wazi yaliyojulikana kama
“88 Grand Open Pool Competitions 2023”, Wanawake mchezaji mmoja mmoja(Singles),
Jackline Tido akicheza dhidi ya mpinzani wake Judith Machafuko(hayupo pichani)
wakati wa fainali iliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Nefaland
Manzese jijini Dar es Salaam.Jackline alishinda 7- 4 na hivyo kuzawadiwa Kikombe Medali ya Dhahabu pamoja na pesa
taslimu shilingi laki tatu(300,000/=).
***********
KLABU ya mchezo wa Pooltable ya Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam imetwaa ubingwa wa mashindano ya Pool ya wazi ya Nane nane yaliyojulikana kama “ 88 Grand Open Pool Competitions 2023” kwa kuifunga timu ya Vegas ya Sinza Dar es Salaam 13-6, yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Nefaland Manzese Agentina Dar es Salaam.
Mshindi wa tatu katika mashindano hayo ni Klabu ya Snipers ya Mwenge Dar es Salaam ambayo iliifunga klabu ya Waturuki ya Temeke 13-6 na hivyo Vegas kuzawadiwa Medali za shaba pamoja na pesa taslimu shilingi elfu hamsini(50,000/=)
Upande wa Wachezaji mmoja mmoja Wanaume(Singles, Abdul Kiande kutoka klabu ya Tiptop alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ya wazi kwa kumfunga Festo Yohana(Tonya) kutoka Tiptop 7-6 na hivyo Kiande kuzawadiwa Kikombe, Medali ya Dhahabu pamoja na Pesa taslimu shilingi laki tano(500,000/=).
Mshindi wa pili Festo Yohana alizawadiwa Medali ya Silva pamoja na pesa taslimu shilingi laki moja(100,000/=)
Mshindi wa tatu ni Seif Hamadi kutoka klabu ya Tiptop ambaye alimfunga Abdallah Hussein kutoka klabu ya Snipers 7-6.Amba Seif Hamadi alizawadiwa medali ya shaba pamoja na pesa taslimu shilingi elfu hamsini(50,000/=)
Upande wa Wanawake Jakline Tido kutoka Dodoma alitetea ubingwa wake kwa kumfunga Judith Machafuko kutoka klabu ya Vegas Sinza Dar es Salaam 7-4 na hivyo Jacline kuzawadiwa Kikombe, medali ya dhahabu pamoja na pesa taslimu shilingi laki tatu(300,000/=)
Judith Machafuko alikamata nafasi ya pili na hivyo kuzawadiwa medali ya silva pamoja na pesa taslimu shilingi laki moja(100,000/=).
Akizungumza mwandishi wetu mara baada ya zoezi la kukabidhi zawadi Mratibu wa Mashindano hayo kwa mara ya nane sasa toka mashindano hayo yaanze kufanyika mwaka 2015, Michael Machela kwanza aliwashukuru Wachezaji na Wadau wote waliojitokeza kushiriki na kushuhudia mashindano ya mwaka huu 2023 ambayo kwa kiasi kikubwa yamefana haijawahi kutokea toka aanze kuratibu.
Alisema Machela jumla ya timu 16 kutoka katika mikoa mbalimbali ilishiriki mashindano hayo,jumla ya wachezaji 110 Wanaume wamefanikiwa kushiriki singles( mchezaji mmoja mmoja) na jumla ya wanawake 16 wamefanikiwa kushiriki singles(mchezaji mmoja mmoja).
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Wilfred Makamba aliwashukuru Wachezaji na Wadau wengi kwa kujitokeza kwa wingi katika mashindano haya lakini pia alipongeza maandalizi mazuri yaliyofanywa na mratibu wa mashindano na mwisho alitoa wito kwa Makampuni na Wadau binafsi kusapoti mchezo wa Pool kwani wachezaji wanajitoa sana kushiriki lakini hamasa ya zawadi haipo bado haijapatikana.
Mwisho aliwashukuru wadau wote waliosaidia kufanikisha mashindano kwa hali na mali na kuwatakia safari njema hususani kwa wachezaji na wadau waliotoka mikoani.









0 comments:
Post a Comment