KIASI cha Shilingi Bilioni 5 kimetengwa na mfuko wa wizara ya sanaa na utamaduni ili kuwawezesha wasanii na waigizaji wa "Bongo Movie" wa mkoa wa Mbeya.
Akizungumza katika kikao maalumu kilichowahusisha
Wasanii, Waigizaji na waimbaji wa mkoa wa Mbeya na Songwe Afisa Mtendaji Mkuu [CEO] wa mfuko huo Nyakaho Mahemba amesema Wizara imeanza kutoa fedha hizo kwa
wasanii kuanzia Desemba 2022 ambapo
imelenga kukuza na kuendeleza kazi za wasanii kujiendesha kibiashara
badala ya burudani pekee.
Mahemba amesema katika mpango wa serikali ni
kuongeza ajira na kuongeza mitaji kwa wasanii kupitia mafunzo na kuongeza
ubora wenye lengo la kukidhi soko la
ndani na nje ya nchi.
Amefafanua kuwa wasanii wana uwezo wa kukopa
mtaji kuanzia Shilingi laki 2 hadi Shilingi Mil 100 ili kufikia malengo na
kwamba mfuko wa Utamaduni unashirikiana na mabenki ili kuwezesha mikopo ya
Wasanii.
Afisa mtendaji Mkuu huyo ameendelea kusema kuwa
tayari imeshatolewa mikopo kwa awamu mbili, mwezi Desemba 2022 na mkopo wa pili
umetolewa Mwezi Februari ambapo tayari
jumla ya Shilingi Bil 1.077 kwa miradi 45 na hivyo kuzalisha ajira
88,750.
Kwa upande wake Afisa Utamaduni wa mkoa wa
Victoria Shao amesema mikopo hiyo ya wasanii itachangia ajira na kuwasaidia
kuwainua kiuchumi ambapo wasanii,waimbaji,wabunifu wa kazi za mikono,Waandishi
wa kazi za kifasihi na wachoraji wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo.











0 comments:
Post a Comment