Nafasi Ya Matangazo

August 24, 2023









Halmashauri ya Chalinze wamepokea gari la Zimamoto na Uokoaji punde yanapotoke majanga hayo wilayani hapo toka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ( SSF) Jenifa Shirima.  

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Chalinze, Mbunge wa jimbo la Chalinze Ndg. Ridhiwani Kikwete amemshukuru Mrakibu mwandamizi kwa niaba ya serikali kwa kuona kuwa katika mipango ya serikali Chalinze nayo iwe moja ya maeneo ya kipaumbele katika uhitaji wa gari hilo. Mbunge alikumbusha kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Chalinze na majanga yaliyo wahi kuwakuta na ujio wa gari hili ni ukombozi mkubwa.

Akizungumza kabla ya kumkabidhi Mbunge wa jimbo hilo, Mrakibu Mwandamizi Jenifa alimpongeza Mbunge kwa kuwasemea wananchi wake na gari hili ni utekeleza wa maombi ya Mbunge na Naibu Waziri Kikwete. 

Mrakibu alimuahidi Mbunge kuendelea kutatua kero za zimamoto katika halmashauri zote mkoa na kwamba na pia kumshukuru Mkurugenzi mtendaji wa Chalinze kwa kuwapatia Kiwanja ambacho watajenga Jengo la zimamoto la wilaya  na ofisi zao. Pia alimuhakikishia Mbunge kuwa serikali inajipanga kwa ajili ya ujio wa gari kubwa wilaya hiyo.

Wananchi wa Chalinze kwa jumla yao wameishukuru Serikali kwa kutatua kero hii ya muda mrefu.  Wameahidi kulitunza. # KaziInaendelea
Posted by MROKI On Thursday, August 24, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo