Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mabalozi kama
ifuatavyo:
i) Amemteua Meja
Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo, Meja Jenerali
Mwaisaka alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji (JWTZ).
ii) Amemteua Meja
Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali
Simuli alikuwa Mkuu wa Utumishi Jeshini (JWTZ).
iii) Amemteua Bw. Mohamed
Awesu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Awesu alikuwa Konseli Mkuu, Konseli
ya Tanzania, Jeddah Saudia Arabia.
iv) Amemteua Bw. Gelasius
Byakanwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Byakanwa alikuwa Afisa Mkuu
Ubalozi wa Tanzania, Korea ya Kusini.
v) Amemteua Dkt. Mohamed
Juma Abdallah kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah alikuwa Katibu
Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja.
vi) Amemteua Bw. Hassan
Mwamweta kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mwamweta alikuwa Afisa Mambo ya
Nje Mwandamizi na Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania, Uturuki.
vii) Amemteua Bw. Imani
Salum Njalikai kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Njalikai alikuwa Afisa wa
Mambo ya Nje Mkuu na Msaidizi wa Waziri Mkuu – Hotuba
viii) Umemteua Bw. Khamis
Mussa Omar kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mussa alikuwa Kaimu Mwakilishi
wa Kudumu, Ubalozi wa Tanzania Ufaransa.
Uteuzi huu wa
Mabalozi umeanza tarehe 10 Mei, 2023 na wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa baadae.
May 22, 2023
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment