Nafasi Ya Matangazo

May 22, 2023

GY3A8679
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Omary Kumbilamoto ameipongeza Kampuni ya Vodacom kushirikiana na Tekno Tanzania kuja na simu aina ya Tecno Camon 20 Series ambazo ni bora kwa matumizi ya mawasiliano na internet.

Ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa simu hiyo, ambapo amewaomba Watanzania kuwa na imani na simu za Tekno ambazo wamekuwa wakizindua kwani wamekuwa wakileta simu ambazo ni bora na imara kwa matumizi.

"Tekno wamekuwa wakijitahidi kuleta simu bora na imara, mimi pia ni mpenzi wa simu za Tekno na hapa nilipo natumia simu ya Tekno, naamini katika ubora wao pia,hivyo nawaomba wananchi wa Dar es Salaam kutumia simu za Tekno kufurahia huduma zilizo bora kabisa". Amesema

Kwa upande wake Meneja Bidhaa za Intaneti - Vodacom Tanzania Samwel Mlole amesema kila Mtanzania ambaye atanunua simu hiyo atazawadiwa 95Gb bure za internet kwa mwaka mzima kwa maana atakuwa anapata 8Gb kila mwezi kwa muda wa miezi 12.

"Ofa hii itampelekea Mtanzania huyu kuweza kupata taarifa mbalimbali na kuweza kujua na kuona faida na uzuri wa hii simu katika angle mbalimbali". Amesema Bw.Mloe

Nae Meneja wa Mafunzo kutoka Tekno Tanzania Bi. Joyce Kaswalala amesema simu hiyo inasifika kuwa na camera nzuri na zimekuja na processor kubwa ambayo inasifika kwa utendaji mzuri wa kazi katika simu.

"Simu hii kwa upande wa Camera inasifika kuchukua picha wakati wa usiku lakini pia picha na video ambazo ziko stable kwasababu imekuja na kitu kinaitwa Sensa shift yenyewe kazi yake kubwa ni kustablize video ambazo zipo katika movement". Amesema
GY3A8740
GY3A8754Meneja Bidhaa za Intaneti - Vodacom Tanzania Samwel Mlole akimueleza jambo MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Omary Kumbilamoto namna simu hizo zilivyo imara,bora na za kisasa kabisa
GY3A8638
Meneja Bidhaa za Intaneti - Vodacom Tanzania Samwel Mlole akitoa ufafanuzi namna Kampuni ya Vodacom Tanzania inavyoshirikiana na Wadau wengine katika mawasiliano,wakati wa hafla fupi uzinduzi uzinduzi wa simu aina ya Tecno Camon 20 Series,uliowakutanisha wadau mbalimbali wa bidhaaa hizo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
GY3A8657
Posted by MROKI On Monday, May 22, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo