Mh.Jaji George Masaju.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wawili kuwa washauri wake.Rais amemteua Jaji George Masaju kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria (Advisor to the President Legal Affairs).
Jaji Masaju ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma. Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Aprili, 2023; na
Pia, Rais amemteua Dkt. Richard Stanslaus Muyungi kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira (Advisor to the President Climate Change and Environment).
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Muyungi alikuwa Meneja wa Mazingira, katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Aprili, 2023.





0 comments:
Post a Comment