Nafasi Ya Matangazo

February 15, 2023

 
Kaimu Mkuu wa Chuo cha ufundi Veta mkoai Mara mwalimu David Luis akizungumza na timu ya wataalam wa mawasiliano kutoka TASAF Makao Makuu waliotmbelea katika chuo hicho ili kuona maendeleo ya wananfuzi 13 wanaotoka katika Kaya Masikini ambao wamefadhiliwa na taasisi hiyokupata mafunzo chuoni hapo
Elly Maduhu ambaye ni mratibu TEA akitoa maelezo kwa maofisa kutoka TASAF Makao makuu pamoja na viongozi wa chuo hicho kuhusu mradi wa TASAF na TEA ambao umesaidia kufadhili wanafunzi mbalimbali kwa ajili yakupata mafunzzo katika chuo hicho.
Mwanafunzi Asha Juma kulia ambaye ni mnafaika na mradi wa TASAF pamoja na TEA pamoja na mwenzake wakiwa katika darasa la kompyuta wakiendelea na mafunzo ya kompyuta.
Muonekano wa Darasa la Kompyuta katika chuo cha Veta mkoani Mara mjini Musoma.
Mwanafunzi Asha Juma kutoka Mtaa wa Matare mjini Musoma ambaye anapata mafunzo ya ufundi bomba katika chuo hicho akiendelea na mafunzo kwa vitendo na mwenzake.
Mwanafunzi Asha Juma kutoka Mtaa wa Matare mjini Musoma ambaye anapata mafunzo ya ufundi bomba katika chuo hicho akiishukuru TASAF kwa kumpatia nafasi ya kusoma katika chuo hicho ambapo ameahidi kutoichezea nafasi hiyona kusoma kwa bidii ilikujikwamua katika hali ngumu ya maisha na umasikini.
Afisa kutoka Dawatila Malalamiko TASAF akizungumza na wanafunzi katika moja ya madarasa ya chuo hicho ambapo amewaasa kusoma kwa bidii ili waweze kupata ujuzi ambao utawasaidia katika maisha yao mara watakapoondoka chuoni hapo nakuingia mtaani.
Picha mbalimbali zikionesha wanafunzi wakiendelea na mafunzo kwa njia ya vitendo katika fani mbalimbali chuoni hapo.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha ufundi Veta mkoai Mara mwalimu David Luis amewashukuru  Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini awamu ya tatu  TASAF kwa jitihada inazozifanya kuwezasha vijana  kupata Ujuzi ambao utawasaidia  kujiajiri au kuajiriwa ili waweze kuendesha maisha yao na familia pamoja na kujitoa kwenye Janga la umaskini.

"TASAF walitulea vijana kumi na tatu (13) ambao hapa chuoni wamegawanyika katika kozi tofauti ambapo katika fani ya compyuter wapo vijana/wanafunzi  wanne(4), umeme wa majumbani wapo wanafunzi watano(5), Fundi Bomba yupo kijana mmoja(1), Ufundi wa magari mwanafunzi mmoja (1), upande wa udereva pia kuna mwanafunzi mmoja(1)," Amesema  Mwalimu David.

Mwalimu David Luis ameyase mahayo wakati akizungumana timu ya wataalam wa mawasiliano kutoka TASAF Makao Makuu waliotembelea katika chuo hicho ili kuona maendeleo ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho baada ya taasisi hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania TEA kuwapeleka wanafunzi 13 kutoka kaya masikini ili kupata ujuzi wa ufundi ili watakapomaliza masomo yao waweze kujiajiri au kupata ajira na kuendesha maisha yao.

Ameongeza kwamba TASAF waliwaletea kiasi cha fedha zaidi ya  shilingi milioni 11 pesa ambazo wanufaika hawa  wanagharamiwa kwenye Ada, nauli na chakula cha mchana wanapokuwa hapa chuoni kwa ajili ya mafunzo.

Aidha Mwalimu David amesema kwamba kuhusu changamoto ya mabweni katika chuo hicho  tayari Serikali kupitia  Bajeti ya fedha ya 2022/2023  ilishawapangia  zaidi ya milion mia tisa (milion 900) ambazo zimetegwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mabweni katika chuo hicho lakini pia wana chuo kingine ambacho kipo katika hatua ya mwisho wilayani Butiama na tayari kina mabweni na kitakapokuwa tayari wataweza kupokea wanafunzi wageni wengi Zaidi.

Kwa upande wake Elly Maduhu ambaye ni mratibu Mamlaka ya Elimu Tanzania TEA mkoani Mara  amesema kwamba mwaka 2010 walibahatika  kupata mradi wa TEA kupitia SDF walipewa kiasi cha shilingi milioni 80 zambazo  waliweza kusajili wanafunzi 280 katika fani ya ufundi wa kompyuta na matumizi ya Kompyuta, wanafunzi wote hao tayari wameshahitimu mafunzo yao na baadhi yao wameajiriwa na wengine wamejiajiri.

Ameongeza kwamba kupitia TASAF waliweza pia kupata mradi kupitia Kaya maskini ambapo wanafunzi kumi na tatu(13) kati yao wanafunzi nane(8) tayari wameanza mafunzo na wengine watawasili kwenye chuo hapo muda si mrefu.

Mwanafunzi Asha Juma ambaye ni mnafaika na mradi wa TASAF pamoja na TEA ametumia nafasi hiyo kutoa shukurani zake kwani kupitia miradi hiyo ameweza kupata mafunzo ambayo yatamsaidia kuajiriwa au kujiajiri na kuendesha maisha yake ya baadae. 

Naye  mabonera  ambaye ni mwanafunzi wa ufundi Seremala  katika chuo hicho ameishukuru TASAF na TEA kwa kumpatia ufadhili wa mafunzo ambapo amewashauri vijana wengine watakaopata nafasi kupitia miradi hiyo kuzitumia nafasi hizo kwa kujifunza kwa bidii kwa ajili ya manufaa yao ya baadae.

Mwanafunzi Asha Juma kutoka Mtaa wa Matare mjini Musoma ambaye anapata mafunzo ya ufundi bomba katika chuo hicho kwa upande wake  ameishukuru TASAF kwa kumpatia nafasi ya kusoma katika chuo hicho ambapo ameahidi kutoichezea nafasi hiyona na kusoma kwa bidii ili kujikwamua katika hali ngumu ya maisha na umasikinikwa maisha yake ya baadaye.
Posted by MROKI On Wednesday, February 15, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo