Nafasi Ya Matangazo

February 13, 2023

Mhandisi mkazi Lutengano Mwandambo akitoa maelezo kwa nodi ya wakurugenzi ya DAWASA kuhusu mradi wa kimkakati wa bwawa la Julius Nyerere- JNHPP.Kulia kwake ni mwenyekiti wa bodi Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange.
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar Es Salaam (DAWASA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi DAWASA, Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa kwenye ziara ya kutembelea  mradi wa Julius Nyerere ikiwa ni utekeleza agizo la Mheshimiwa Raisi, Dkt Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati akizindua zoezi la ujazaji maji bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere.
*********
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar Es Salaam (DAWASA) imepongeza maendeleo ya utekelezaji ujenzi  mradi wa kimkakati wa kufua umeme kwa maji wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha jumla ya megawati 2,115 uliofikia asilimia 81.82 hadi kufikia tarehe 31 Januari 2023.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi DAWASA, Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa ziara ya kutembelea  mradi wa Julius Nyerere ikiwa ni kitekeleza agizo la Mheshimiwa Raisi, Dkt Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati akizindua zoezi la ujazaji maji bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere.

"Mhe. Rais alituagiza sisi DAWASA tunufaike kupitia maji ya mto Rufiji kwa kusambaza maji safi na salama kwa wakazi wa mikoa ya Dar-Es-Salaam na Pwani baada ya kuwa yamezalisha umeme" alisema Jenerali Mwamunyange.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja amepongeza kazi nzuri iliyofanyika kwenye mradi huo  na amefurahi  ushirikiano  mkubwa uliopo kati yao (DAWASA) na TANESCO.

Awali Mhandisi Mkazi Lutengano Mwandambo alieleza kuwa zoezi la ujazaji maji linaendelea vizuri na limefikia mita za  ujazo 131.02 kutoka usawa wa bahari.
Posted by MROKI On Monday, February 13, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo