Nafasi Ya Matangazo

February 10, 2023

Naibu Waziri katika ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi (wa nne kutoka kushoto) akipokea kitabu cha Mwongozo kwa Mwanachama kutoka kwa Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (wa pili kushoto), wakati alipotembelea banda la PSSSF katika Maadhimisho ya miaka kumi ya e-GA, jijini Arusha. Wa tano kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa e-GA, Mhandisi Benedict Ndomba.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa PSSSF kanda ya Kaskazini-Arusha. Kutoka kushoto ni Bi. Hadia Hongoa, Meneja wa PSSSF kanda ya kaskazini Bi. Vonness Koka na Bi. Cleopatra Luze, wakati wa sherehe za miaka kumi ya e-GA.
Naibu Waziri katika ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, tuzo kwa ajili ya kufanikisha sherehe za miaka kumi ya e-GA na kikao kazi cha tatu cha serikali mtandao. kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro, katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa e-GA, Mhandisi Benedict Ndomba.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Naibu Waziri katika ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi amezipongeza baadhi ya taasisi za umma, ukiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuweza kuwafikia wananchi kiurahisi kwa kutumia matumizi ya TEHAMA.
Mheshimiwa Ndejembi aliyasema hayo jijini hapa katika hotuba yake ya ufunguzi sherehe za kutimiza miaka kumi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na kikao kazi cha tatu cha serikali mtandao, kinachokutanisha wataalam wa TEHAMA kutoka serikalini.

“Leo nimejionea kwenye mabanda pale PSSSF wameweza kuweka App ili kuweza kuona michango inavyokwenda Hivyo nielekeze e-GA kuendelea kufanya tafiti ili kuleta bunifu za mifumo ya TEHAMA itakayoliwezesha taifa kufanikiwa kuimarisha sekta za viwanda, biashara na uwekezaji kulipeleka mbele taifa letu kimaendeleo. 
Na katika hili nitoe pongezi pia kwa taasisi ambazo tayari zimeweza kuwafikia wananchi kiurahisi Zaidi na kuondoa urasimu wa makaratasi…” alisema Mhe. Ndejembi.

Mheshimiwa Ndejembi amezishauri taasisi nyingine za umma kuitumia TEHAMA ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za serikali kwa haraka.

PSSSF ina huduma za PSSSF Kiganjani na PSSSF Mtandaon. Huduma hizi ni suluhisho kwa wanachama, wastaafu na waajiri kuweza kupata huduma popote walipo na muda wowote kwa kutumia simu janja au kompyuta bila kuhitaji kufika kwenye ofisi za PSSSF.
Posted by MROKI On Friday, February 10, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo