Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Airtel Money Daudi Ndovu (kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam wakati anatangaza kuanza kutoa Gawio la faida la Airtel Money ambapo kiasi cha Tzs 1.6 bilioni kitatolewa kwa wateja na mawakala. Pamoja nae ni Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Airtel, Jackson Mmbando.
********
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel Tanzania leo imetangaza kutoa faida ya Tzs 1.6 bilioni kwa wateja na
mawakala ambao wamekuwa wakitumia huduma ya Airtel Money kwa kipindi cha Julai
mpaka Septemba 2022. Airtel kupitia Airtel Money imekuwa ikitoa faida hii kwa
wateja na mawakala baada ya kuidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Faida ya Gawio la Airtel Money hutolewa kwa wateja, wadau na mawakala wa Airtel Money kwa kila robo ya mwaka kulingana na kiasi kilichopo kwenye akaunti zao za Airtel Money.
Kiasi cha
faida ambacho mteja au Wakala unachopata hutegemea na jinsi ambavyo unatumia
huduma za Airtel Money na faida hii huwekewa moja kwa moja kwenye akaunti yako ya Airtel Money ambapo mteja au Wakala unaweza
kuitumia kwenye matumizi ya kawaida kama
vile kutoa au kutuma fedha, kufanya malipo ya huduma kama DAWASCO, LUKU au
huduma zingine kulingana na vile unavyotaka.
Akizungumza leo jijini Dar es
Salaam wakati anatangaza kuanza kutoa Gawio la faida la Airtel Money, Mkuu wa
Kitengo cha Huduma za Airtel Money Daudi Ndovu alisema, “Gawio la Faida la
Airtel Money hili litatolewa kwa wateja na Mawakala wote ambao walikuwa
wakitumia huduma za Airtel Money kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2022 kote nchini kuanzia leo”.
“Dhamira yetu ni kuendelea kuunga mkono juhudi
za serikali ya kupanua huduma za kifedha kwa ujumuhishi. Leo tunatangaza kuanza
kugawa faida ya gawio la Airtel Money la Tzs 1.6 bilioni kwa wateja na mawakala
wa huduma za Airtel Money kote nchini. Tunayo furaha kuona ni jinsi gani huduma
ya Airtel Money inavyozidi kukua hapa nchini.” alisema Ndovu
Ndovu aliongeza ‘Airtel
imedhamiria kuendelea kuboresha na kuleta huduma za Airtel Money karibu na
wateja na kufikia Watanzania ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki hasa maeneo ya vijijini. Na ili kuendelea kukuza
huduma kifedha jumuishi, Airtel Money imeweza kuzindua promosheni ya Bila Tozo
ambapo kwa sasa wateja wanaweza kutuma au kutoa fedha BILA TOZO na hivyo
kuendelea kukuza biashara kwa kufanya malipo kwa unafuu zaidi.
Airtel itaendelea kuleta bidhaa na huduma
zenye kutoa masuluhisho kwa watanzania kila wakati ikiwemo kutuma au kutoa fedha pamoja na
kufanya malipo kwa njia ya mtandao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kuwa Airtel inaendelea na dhamira yake ya kuwekeza kwenye kupanua wigo wa mtandao wa Airtel Money ili kuendelea kutoa huduma zilizo bora zaidi.
“Tunayo furaha kwamba kwa sasa tumejipanaga
vyema kwa kuweka miundombinu bora ya usambazaji wa huduma zetu za Airtel Money
yakiwemo maduka ya Airtel Money Branch zaidi ya 3,500 kote nchini pamoja na
Mawakala wa Airtel Money waliosambaa nchi nzima zaidi ya 170,000.”
Tutaendela kutoa huduma iliyo
bora ili kuhakikisha kuwa wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma zetu kila
kona saa 24 / siku 7 za wiki aidha
wakiwa nyumbani au ofisini.
0 comments:
Post a Comment