Mwenyekiti wa madereva Bajaji Manispaa ya Iringa Melabu Kihwele akiwa katika ya madereva Bajaji wa Manispaa ya Iringa alipowatembelea katika vituo vya Bajaji kutoa elimu ya kupinga vikali vitendo vya ukatili wa kijinsia
Mwenyekiti wa madereva Bajaji Manispaa ya Iringa Melabu Kihwele akiwa katika ya madereva Bajaji wa Manispaa ya Iringa alipowatembelea katika vituo vya Bajaji kutoa elimu ya kupinga vikali vitendo vya ukatili wa kijinsia
***************
Na Fredy Mgunda, Iringa.
MWENYEKITI wa chama cha madereva Bajaji Manispaa ya Iringa Melabu Kihwele amewataka madereva Bajaji kuacha kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa abiria ambao wanawapakia.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea vituo vya Bajaji Manispaa ya Iringa, mwenyekiti huyu Melabu Kihwele alisema kuwa uongozi wa Bajaji Manispaa ya Iringa hautamvumilia Dereva Bajaji yoyote yule ambaye anafanya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Kihwele alisema kuwa wanaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupinga vikali vitendo vya ukatili kwa Watoto na wanawake ambavyo kwa siku za hivi karibu vimezidi kuongezeka.
Alisema kuwa Dereva Bajaji yoyote atakaye baka au kulawiti hawatamfumbia macho kwa kuharibu taswira ya madereva Bajaji Manispaa ya Iringa.
Kihwele alisema kuwa kubaka, kulawiti na kuaafanyia ukatili wanawake hukumu take ni kifungo cha miaka 30 jela hivyo madereva Bajaji Manispaa ya Iringa wanatakiwa kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
"Hivi karibuni si kuna Dereva Bajaji wa hapa Manispaa ya Iringa amefungwa miaka 30 jera kwa kosa la ukatili wa kijinsia kwa mtoto wa kike si ndio hivyo serikali ikitaka ushirikiano na uongozi wa Bajaji Manispaa ya Iringa sisi tupo tayari"alisema Kihwele
Mwenyekiti wa madereva Bajaji Manispaa ya Iringa Melabu Kihwele alimazia kwa kusema kuwa jamii ya watanzania hawajazoea vitendo vya ukatili wa kijinsia kufanywa na madereva Bajaji hivyo Dereva Bajaji yoyote atakaye kutwa na tuhuma au kesi hiyo uongozi hauwezi kumsaidia.
0 comments:
Post a Comment