Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifunga mafunzo ya Sanaa ya Uongozi (The Art of Leadership) kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) yaliyotolewa na Taasisi ya UONGOZI jijini Dodoma.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Michael Mwakamo (wa kwanza kushoto) akiwa na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya USEMI, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati Waziri huyo akifunga mafunzo ya Sanaa ya Uongozi (The Art of Leadership) yaliyotolewa na Taasisi ya UONGOZI kwa wajumbe wa kamati hiyo jijini Dodoma.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (aliyesimama) wakati waziri huyo akifunga mafunzo ya Sanaa ya Uongozi (The Art of Leadership) yaliyotolewa na Taasisi ya UONGOZI jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya USEMI ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Makete, Mhe. Festo Sanga akieleza faida ya mafunzo ya Sanaa ya Uongozi (The Art of Leadership), waliyopatiwa na Taasisi ya UONGOZI jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji.
Mjumbe wa Kamati ya USEMI, Dkt. Alice Kaijage akieleza namna wajumbe wa Kamati ya USEMI walivyonufaika na Mafunzo ya Sanaa ya Uongozi (The Art of Leadership), waliyopatiwa na Taasisi ya UONGOZI jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya USEMI na baadhi ya Watendaji wa Serikali, mara baada ya waziri huyo kufunga mafunzo ya Sanaa ya Uongozi (The Art of Leadership) yaliyotolewa na Taasisi ya UONGOZI kwa wajumbe wa kamati hiyo jijini Dodoma.










0 comments:
Post a Comment